Nchi ya Tanzania imejitolea na kuwa na mipango endelevu katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kupitia sera na mipanho mbalimbali iliyowekwa katika utekelezaji
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji wakati akizungumza kwenye Jukwaa la 24 na Mkutano wa 35 wa Kamati ya Kudumu ua Fedha ya Mkataba wa Mabadiliko ya Tabia Nchi (UNFCCC), uliofanyika kwenye Kituo cha Kitamataifa cha Mikutano AICC ukumbi wa Simba Septemba 2, 2024.
Mhe. Dkt. Kijaji amesema kuwa, athari za mabadiliko ya tabia nchi yanayosababisha mabadiliko ya hali ya hewa, ongezeko la joto, mvua zisizo za kawaida, dhoruba za kitropiki na mafuriko makubwa yanayoathiri uchumi na mifumo ya ikolojia za kijamii, zinahitaji juhudi za ziada na timu kuhwa inayojitoa kukabiliana nayo.
"Changamoto hizi zinasababisha hasara kubwa na uharibifu wa miundombinu muhimu ya maji, barabara, umeme na kilimo na kusababisha uhaba wa maji na chakula kwa matumizi ya binadamu na wanyama hivyo juhudi kubwa zinahitajika kukabilina na mabadiliko ya tabianchi" Amesema Dkt. Kijaji.
Licha ya kuwa Tanzania inajivunia kuwa mwenyeji wa mkutano huu muhimu, Tanzania imejitolea katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, kupitia sera mbalimbali ikiwa ni pamoja na Sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021, Mpango Mkuu wa Mazingira wa Kitaifa wa Miaka ya Mkakati kutoka mwaka 2022 hadi 2032, pamoja na Sera ya Taifa ya Uchumi wa Buluu ya mwaka 2024, na kuwa na mradi endelevu wa kupunguza athari za hali ya hewa.
Uimarishaji wa hali ya hewa katika maeneo yaliyoathirika na mafuriko, kukuza teknolojia za kupikia kwa kuhimiza matumizi ya nishati safi, kutekeleza usimamizi endelevu wa ardhi,kuimarisha maeneo ya pwani yanayokabiliwa na kupanda kwa kiwango cha bahari, mafuriko, na erosheni ya fukwe, kufungua uwezo wa uchumi wa buluu katika mifumo ya ikolojia ya pwani na baharini.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.