Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan amesema, Serikali ya awamu ya sita imejipanga kuhakikisha ifikapo 2025 miji yote itakuwa na umeme kwa asilimia 100 na baadhi ya maeneo kuwa na umeme kwa asilimia 85 hadi 95.
Kauli hiyo, ameitoa alipokuwa akizungumza na wananchi wa Jiji la Arusha katika eneo la kona ya Mbauda alipokuwa akiwasili Mkoani humo.
Amesema, bado kuna miradi mbalimbali ambayo Serikali inaendelea kuitekeleza itakayo saidia kuongeza kiwango cha umeme likiwemo bwala la Julias Nyerere.
Miradi hiyo ikikamilika itaondoa tatizo la kukatika umeme mara kwa mara ambalo lipo sasa.
Mhe.Samia amewasili Mkoani Arusha akitokea Mkoa wa Manyara alipokuwa na ziara ya Kikazi na ataendelea na ziara ya Kikazi katika Mkoa wa Arusha kwa siku 4.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.