Ni wajibu wa kila mtu kushiriki katika vita hii dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya hasa katika kuhakikisha watumiaji wanapatiwa tiba hasa kwa kushirikisha wadau mbalimbali.
Akitoa rai hii alipokua akifungua semina ya mpango wa kuboresha na kuanzishwa kwa huduma za tiba dhidi ya dawa za kulevya kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo. Katibu tawala wa mkoa wa Arusha Richard Kwitega amesema ni vizuri viongozi wakajikita kwa nguvu zote katika zoezi hili lakutokomeza ugonjwa wa madawa ya kulevya kwenye maeneo ya Arusha na nchini kiujumla.
“Kila kiongozi ahakikishe anasimamia vyema uwazishwaji wa huduma hii ya tiba kwa watumiaji wa dawa za kulevya ili kuweza kunusuru kizazi hiki”.
Kwa mujibu wa tafiti ya mwaka 2014 watu takribani 250,000 hadi 500,000 ndio wanatumia dawa za kulevya hususani Heroine.
Akisisitiza zaidi Kamishina msaidizi mamlaka ya kudhibiti dawa za kulenya Daktari Peter Mfisi, amesema dawa nyingi zinazotumika katika nchi yetu ni pamoja na vichangamshi ,vipumbaza,na vileta njozi.
Watumiaji wakubwa wa dawa hizi ni wenye umri kati ya miaka 10 hadi 12 na wazee wenye umri wa miaka 60 na kuendelea.
Madhara makubwa wanayoyapa ni pamoja nakupata magonjwa ya ngozi,maambukizi ya HIV, magonjwa ya akili,sekta za kiafya ,kijamii,kiuchumi,kimazingira,na kiusalama.Hivyo swala la uthibiti linahitaji ushirikiano wa watu wote kiujumla katika kutoa elimu kuharibu mashamba na upimaji pamoja na kinga
Akitoa sababu zinazofanya watu kutumia madawa ya kulevya sana ni pamoja na msukumo rika, migogoro ya kifamilia ,kukosa malezi bora ,uelewa mdogo wa stadi za maisha ,ukosefu wa kazi , kutokujua madhara yake pia wengine ni kwa sababu ya upatikanaji kirahisi mfano bangi.
Huku akieleza vyanzo vya dawa hizi za kulevya ni pamoja na usafirishaji mfano cocaine inatokea sana Afrika magharibi na kusini pia mirungi inatokea sana Kenya pia uchepushaji ,utendenezaji,akisema hii mara nyingi hufanyika kwenya mahabara feki.
Nae mratibu wa matumizi ya dawa za kulevya kutoka wizara ya afya,maendeleo ya jamii, jinisia ,wazee na watoto Daktari Neema Makyao, amesema takwimu na uhusiano uliopo kati ya maambukizi ya Ukimwi na madawa ya kulevya .milioni 37 watu wanaoishi na Ukimwi ulimwenguni,milioni 1.8 wanaambukizwa na milioni19.4 wanaishi na VVU na kila mwaka takribani watu 81,020 wanaambukizwa VVU .Tanzania 4.7% na 6.5%wanawake na 3.5% wanaume. Na kwa Arusha maambukizi ni 1.9.
kuna uhusiano mkubwa baina ya matumizi ya dawa za kulenya na maambukizi ya VVU, kwani watumiaji wa dawa za kulenya kwa kiasi kikubwa wapo kwenye uwezekano mkubwa wakuambukizwa VVU.
Amesema watumiaji wa dawa za kulevya kwa sindano ndio wapo kwenye hatari kubwa yakupata maambukizi ya VVU kwani wengi wao hutumia sindano ambazo si salama kwa afya zao.
Ameeleza pia jinsi ya kuwatambua wagonjwa hawa au wahathirika hawa ni pamoja na mabadiliko ya tabia ,tabia za kujitegemea ,udokozi na kukosa hamu ya kula pamoja na nyingine nyingi zisizo za kawaida. Amesema Nchini matumizi ya bangi yamekua makubwazaid ,gongo za kichina na ongezeko la dawa za hospital.
Semina hii itakua inafanyika kila mwaka kwa lengo la kuhamasisha jamii kuifahamu MAT (Methadone Assisted Therapy),jinsi ya kuwatambua walengwa ,wadau katika kikao jinsi ya kutoa elimu na kutambua mipango madhubuti katika kujikimu kwa waathirika.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.