Na Elinipa Lupembe.
Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimeanza Kampeni rasmi ya kitaifa ya kwenye mikoa ya kanda ya Kaskazini ya Arusha, Kilimanjaro na Tanga ya kuhamasisha watanzania kuchangamkia fursa za uwekezaji kwa kuwekeza katika miradi mbalimbali nchini.
Akizungumza mkoani Arusha, alipotembelea Kampuni ya Hanspaul ya jijini Arusha, Meneja Uhamasishaji Uwekezaji wa ndani, Kituo cha UwekezajiTanzania, Felix John, amesema kuwa, TIC imeanza Kampeni ya kitaifa ya kuhamasisha watanzania wazawa kuwekeza nchini.
Amesema kuwa Kampeni hiyo, ina malengo makuu mawili ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kuhusu dhana ya uwekezaji, kuwahamasisha watanzania kushiriki katika na kuondoa fikra na mtazamo potofu kwa watanzania kwamba wawekezaji ni wageni kutoka nje ya nchi.
Ameweka wazi kuwa, Serikali kupitia, Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara,kwa kushirikiana na TIC, imeshusha kiwango cha fedha za uwekezaji kwa wazawa kutoka Dola za Kimarekani 100,000 hadi kufikia 50,000 sawa na Shilingi milioni 125 ili kuwavutiwa wawekezaji wa ndani kuwekeza na kusajili miradi yao.
Amesema kampeni hiyo,imelenga kutekeleza malengo makuu mawili ikiwamo kutoa elimu kwa Watanzania kuhusu dhana ya uwekezaji pamoja na kuwahamasisha kushiriki kikamilifu kwa kuwekeza katika miradi mbalimbali ya kiuchumi na kuchangamkia fursa zilizoko.
Naye Mkurugenzi wa Kampuni ya Hanspaul inayotengeneza magari ya utalii, na mwekezaji wa ndani, Satbir Singh Hanspaul, ameipongeza serikali kwa kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji kwa wawekezaji wa ndani na nje.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.