Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Dkt. Athumani Kihamia ameitaka Halmashauri ya Monduli kuhakikisha ina tenga 40% ya mapato yake kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo.
Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza kwenye kikao cha kujadili hoja za mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali katika Halmashauri ya Monduli.
Dkt. Kihamia amesema kwa Halmashauri kushindwa kutenga hizo fedha ni kuwakatisha tamaa wananchi wanao anzisha miradi ya maendeleo kama vile ujenzi wa shule na vituo vya Afya.
Fedha hizo zinasaidia kumalizia miradi kama hiyo iliyoanzishwa na wananchi, hivyo kutozitenga ni kisababisha miradi hiyo kukwama.
Mwenyekiti wa halmashauri ya Monduli Mhe. Isack Copriano, amesema baraza la madiwa litahakikisha linasimamia miradi yote ya maendeleo kwa ustawi wa wilaya hiyo.
Pia, atahakikisha fedha zote za halmashauri zinatumika kama ilivyopangwa hasa za asilimia 40 za maendeleo.
Mkurugenzi wa halmashauri ya Monduli Ulaya Anderson amemuhakikishia Katibu Tawala kuwa watafanya kazi kwa makini ili kuepuka hoja zisizo na ulazima katika Halmashauri hiyo.
Dkt. Kihamia anaendelea na ziara yake katika Halmashauri za Mkoa wa Arusha ya kusikiliza hoja za mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali na kutoa maelekezo mbalimbali ambayo yatasaidia Halmashauri hizo kuendelea kuwa na hati safi.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.