Viongozi wa Taasis za Serikali Mkoani Arusha, wametakiwa kufanya kazi kwa umoja na mshikamano, katika kuhakikisha wanatoa huduma shahiki kwa wananchi.
Maelekezo hayo yametolewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mheshimiwa Idd Kimanta alipokutana na viongozi hao na kujitambulisha kwao kama kiongozi wao mpya, jijini Arusha.
“Siri kubwa ya mafanikio ni kufanya kazi kwa umoja na kujenga hali shirikishi katika taasis zenu ndipo mtakapoweza kufikia malengo mliojipangia”.
Baadhi ya viongozi kutoka taasis mbalimbali za serikali mkoani Arusha, wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Arusha (Hayupo pichani) katika
kikao kazi kilichofanyika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Mheshimiwa Kimanta amewashauri kutopenda kutumia lugha za umri sana kwa wasaidizi wao, bali watumie mbinu ya kujenga mahusiano mazuri ya kazi kwani hata wao wanajitambua na wanaelewa wajibu wao katika kutekeleza majukumu yao.
Amewataka viongozi hao wakafanye kazi kwa utulivu, na ili waweze kufanikisha hilo wajitaidi kupata taarifa nyingi zinazohusu taasis zao na wasaidizi wao ambazo zitawasaidia kujenga zaidi nguvu na mshikamano.
Pia, amewashauri kwenda kusimamia misingi na taratibu za uongozi wa taasis zao bila kuogopa changamoto zozote zitakazoibuka na wakishindwa basi wasisite kumshirikisha yeye kwa msaada zaidi.
Amesisitiza zaidi kuwa kila kiongozi wa taasis ya serikali ni mteule wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hivyo hawana budi kuhakikisha wanatekeleza yale yote ambayo Rais anayataka katika kuleta maendeleo ya nchi.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Arusha mheshimiwa Kenan Kihongosi, amesema yote yaliyozungumzwa na Mkuu wa Mkoa ni maelekezo kwa viongozi wote wa serikali hivyo wanatakiwa kuyafanyia kazi.
Aidha, amewataka viongozi hao wa taasis za serikali kuchukua hayo maelekezo na kuyafikisha kwa wasaidizi wao wa ngazi za chini hii itasaidia kuongeza ufanisi zaidi mahala pao pa kazi.
Mkurugenzi wa huduma za ufundi kutoka taasis ya utafiti wa viwatilifu katika ukanda wa Kitropiki (TPRI) daktari Efrem Njau, amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kuwapa muongozi mzuri wa namna ya kufanya kazi kwa umoja katika mkoa wa Arusha.
Daktari Njau amesema, watawashirikisha wanao waongoza yale yote walioelekezwa na Mkuu wa Mkoa kwa kuongeza ufanisi zaidi katika taasis zao.
Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi kutoka Taasis ya Utafiti wa Viwatilifu katika Ukanda wa Kitropiki, Daktari
Efrem Njau, akizungumza katika kikao kazi cha wakuu wa Taasis za serikali za Mkoa wa Arusha,jijini Arusha.
Mkurugenzi kutoka walaka wa barabara(TANROAD) Arusha, Inginia Johnny Kalupale amesema, wao kama viongozi wa taasis za serikali wapo tayari kutoa ushirikiano kwa Mkuu wa Mkoa ili kuhakikisha Mkoa unatekeleza yale yote ambayo Mheshimiwa Rais anayataka.
Mheshimiwa Kimanta amekutana na viongozi hao wa taasis za serikali kwa lengo kubwa la kujitambulisha kwao na kuwapa muongozo wa namna ya kutekeleza majukumu yao ndani ya Mkoa wa Arusha.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.