" Vijana wa Kitanzania wametakiwa kuchangamkia fursa ya mafunzo ya ukarimu pale inapotokea nafasi kama hizo ili kukuza soko la ajira kwa vijana hao".
Yamesemwa hayo na Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Dkt. Athumani Kihamia alipokuwa akikabidhi vyeti kwa wahitimu 111 wa mafunzo ya Uanagenzi katika chuo cha Taifa cha utalii kampasi ya Arusha.
Amesema Serikali iliona kuna haja ya kuongeza wigo wa fursa za ajira kwa Taifa.
Amesisitiza zaidi kuwa mafunzo hayo yamewasaidia kuwajengea kwa kiasi kikubwa vijana wa Kitanzania kuongeza ujuzi na ubunifu katika sekta ya ukarimu.
Mafunzo ya Uanagenzi yamedhaminiwa na ofisi ya Waziri Mkuu- Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye ulemavu.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.