Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Iddi Hassan Kimanta ameridhishwa na namna ujenzi wa majengo ya afya na shule katika wilaya ya Longido.
Kimanta ameyasema hayo alipokuwa akikagua miradi ya maendeleo katika wilayani hiyo na kuwapongeza kwa juhudi walizozifanya katika usimamizi.
Aidha, Kimanta ametoa wito kwa Halmashauri zote za Mkoa wa Arusha watumie wajenzi wa kawaida katika kujenga miundombinu ya maendeleo hasa pale inapotakiwa kufanya hivyo ili kupunguza gharama za ujenzi.
Amewasisitiza kuendelea kusimamia miradi hiyo kwani serikali inatoa fedha nyingi ili kuleta maendeleo kwa wananchi.
Nae, Mkuu wa Wilaya ya Longido Mhe. Frank Mwaisombe amesema wilaya itaendelea kusimamia miradi kwa ukaribu zaidi ili kuwaletea maendeleo wananchi.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha yupo katika ziara ya siku 2 wilayani humo akikagua miradi ya maendeleo katika sekta ya afya na elimu.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.