Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan amezita taasisi za Serikali na binafsi kutumia teknolojia katika utunzaji wa kumbukumbu na nyaraka.
Kauli hiyo, ameitoa alipokuwa akifungua Mkutano Mkuu wa 10 wa chama cha Taaluma ya Menenjimenti ya kumbukumbu ya Nyaraka Tanzania, Jijini Arusha.
Kwakutumia teknolojia itasaidia kupunguza msongamano na kurahisisha kazi.
Aidha, amewataka watunza kumbukumbu hao kuendelea kufanya kazi kwa weredi, uadilifu huku wakitunza siri kwani wao ndio kama roho ya utendaji serikalini.
Mhe.Samia amemaliza ziara yake ya kikazi ya siku 4 Mkoani Arusha.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.