Mkuu wa Wilaya ya Karatu Dadi Kolimba amewataka wananchi wa Karatu hususani wanaofanya kazi za kilimo katika bonde la Eyasi kutunza miti iliyopandwa kwa lengo la kulinda chanzo hicho cha Maji.
Amesema hayo alipokuwa akizundua zoezi la upandaji Miti katika Wilaya hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongella.
Amesema wameamua kupanda miti takribani 1000 ili kuunga Mkono juhudi za Rais wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia za kulinda mazingira lakini pia kulinda vyanzo vya Maji.
Chanzo hicho cha maji kimekuwa kikiwasaidia wakulima wa vitunguu katika bonde la Mto.Baray.
Aidha, amemtaka afisa Mazingira wa halamshauri hiyo kifanya tathimini za wale wote watakaoharibu mazingira ya bonde hilo ili sheria kali ichukuliwe dhidi yao.
Mwenyekiti wa halmashauri ya Karatu Dkt. John Mahu amesema halmashauri hiyo imetenga kiasi cha Milioni 54 kwa ajili ya upandaji Miti katika maeneo mbalimbali.
Pia, itasimamia miti yote ipandwe kwa wakati na kuendelea kutuzwa.
Nae, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Karatu bwana Karia Rajabu amesema swala la upandaji miti ni endelevu na watendeja wote watakagua maeneo yote ambayo miti itapandwa ili kuhakikisha inastawi na kutunzwa vizuri .
Zoezi la upandaji Miti katika halmashauri ya Karatu ni mwendelezo wa kuhakikisha inatimiza lengo la kupanda miti 1,500,000 kwa mwaka 2022/2023.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.