Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.John Mongella ametoa wito kwa madhehebu yote ya kikristo kushirikiana na Serikali katika mapambano ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwani serikali inatambua juhudi zinazofanywa na madhehebu hayo.
Ametoa wito huo alipokuwa akizungumza na wananchi wa Jiji la Arusha katika kongamano la siku ya UKIMWI duniani lililoandaliwa na Halmashauri ya Jiji la Arusha.
Amesema UKIMWI kwa kiasi kikubwa unaambukizwa kwa njia ya ngono zembe hivyo ni hatua za kujikinga zinaitajika zaidi.
Aidha, amewahasa wanaume wajitokeze kupima kwa wingi kwani hadi sasa idadi kubwa ya wanaopima ni wanawake.
Nae, Afisa maendeleo ya Jamii Jiji la Arusha bi.Tajiel Mahega amesema,katika kuadhimisha miaka 60 ya Uhuru wameanzisha kampeni ya kupima virusi vya UKIMWI na jumla ya watu 370,603 wamepima na kati yao watu 2250 waligundulika wameambukizwa virusi hivyo.
Katika Jiji la Arusha kiwango cha maambukizi kimepanda kutoka asilimia 2.3 mwaka 2019/2020 hadi asilimia 2.8 mwaka 2020/ 2021.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.