Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella amesema atashirikiana na wananchi wa Mkoa wa Arusha katika kuleta maendeleo ya Mkoa mzima.
Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na makundi mbalimbali ya kijamii ya Mkoa wa Arusha.
Amesema anapenda maendeleo ya Mkoa yawe ni agenda ya kila mwananchi wa Mkoa wa Arusha.
Maendeleo ya Mkoa wa Arusha yataletwa na Mshikamano na umoja kwa wananchi wote wa Mkoa wa Arusha.
RC Mongella,amekutana na kufanya kikao na makundi mbalimbali ya kijamii ya Mkoa wa Arusha yakiwemo Viongozi wa dini, wafanyabiashara na taasisi za kiserikali.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.