Timu iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha ,Mrisho Gambo kwa kushirikiana na vikosi vya ulinzi na usalama imebaini kuuwawa kwa Twiga 35 kwa kipindi cha miaka miwili katika matukio mbalimbali ikiwemo ujangili.
Aidha Twiga 25 kati ya hao wameuliwa kutokana na vitendo vya ujangili wa kitoweo pamoja na imani kuwa mafuta ya twiga ni dawa ya kutibu magonjwa mbalimbali .
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Mkuu wa Mkoa wa Arusha alisema kufuatia mauaji ya twiga hao aliunda kamati maalum kwaajili ya kuchunguza matukio hayo ikishirikiana na vikosi mbalimbali viwemo Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) , Mamlaka ya Hifadhi ya Wanaymapori (TAWA) ,Kikosi Dhidi ya Ujangali Kanda ya Kaskazini (KDU) Jeshi la Polisi pamoja na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ili kubaini ni kwanini mauaji ya wanyama hao yametokea katika kipindi cha miaka miwili na ndani ya mwaka mmoja mwaka 2018 twiga 24 waliuawa kwaajili ya ujangali huku mwingine akifa baada ya kugongwa.
Alisema mara baada ya kuunda timu hiyo Afisa wa KDU Kanda ya Kanda ya Kaskazini , Said Mkeni alionekana kutoa taarifa kwa majangili juu ya kamati inachofanya ndipo alipopata taarifa juu ya afisa huyo na kumpigia simu Katibu.
Alisema pia timu hiyo ilipewa hadidu za rejea sita ikiwemo kufutilia vielelezo ikiwemo wakili mfawidhi wa Mkoa wa Arusha kuongeza kasi ya kisheria ili kuwezesha kesi kupangwa mahakamani ili ziende haraka, kuitisha na kusoma majalada ili kubaini mashauri yaliyofunguliwa mahakamani au polisi
Kujua jinsi watuhumiwa wanavyoachiwa mahakamani, wafadhili na masoko ya wanyama hao, kuchunguza matukio ya ujangili ,Afisa wanyamapori KDU kuchukuliwa hatua kutokana na tabia yake ya kuhujumu kazi za kamati.
Alisema mara baada ya kupokea taarifa hiyo aliijulisha Wizara ya Maliasili na Utalii na ndipo Januari 4 ,2019 Waziri wa Maliasiali na Utalii, Dk, Khamis Kigwangwala walimsimamisha kazi Mkuu wa KDU badala yake aliletwa Nassoro Salumu.
Rc Gambo alisema katika tume hiyo wamebaini kuwa majalada ya kesi 27 yaliyopo mahakamani yapo katika hatua za kutajwa na matatu kati ya hayo niya ujangili wa twiga, matatu meno ya tembo na 19 ni ujangili wa wanyama wengine .
Pia kamati imegundua majalada hayo kutoandaliwa vizuri na udhaifu mkubwa upo katika Kikosi cha Kuzuia Ujangili (KDU) na Ofisi ya Afisa Wanyamapori Wilaya ya Longido hawafanyi kazi zao ipasavyo.
KDU wanaonekana wakati wa matukio ya ujangali yanapotokea na Afisa Wanyamapori analalamikia kutokuwa na usafiri wakati serikali imetoa gari kwaajili ya doria hivyo baada ya uchambuzi wa kina kamati imebaini katika kipindi cha miaka miwili twiga 25 walikufa na mwaka 2018 twiga 24 na mwaka 2017 twiga mmoja na kwa mwaka 2018 tiga wawili waliuliwa kawasababu ya ujangili kila mwezi.
Ofisi za KDU wanasema walikufa twiga watatu na Afisa wanyamapori anadai twiga sita walikufa sasa taarifa zinakinzana na Kamati imebaini KDU na Ofisi ya Afisa Wanyamapori wilaya ya Longido hawatekelezi majukumu yao ipasavyo.
“KDU wanaonekana pale kunapotokea mizoga ya wanyama matukio ya ujangili yanayoripotiwa na DGO analalamikia kutofika kwa wakati kwenye tukio wakati serikali imetoa gari jipya namba STL 6217 Land Cruiser mwanzoni mwa mwaka 2018 “
Alisema baada ya uchambuzi wa kina kamati imebaini twiga hao walikufa kwasababu mbalimbali ikiwemo ujangili 25, 2 mafuriko na 2 shoti ya umeme, mmoja kutumbukia kwenye korongo huku Kamati iyoundwa imebaini twiga 25 kuuwa na taarifa zingine hazijaenda mahakamani kwasababu ya vikosi hivyo viwili kutokuwa waadilifu .
“Twiga wanakufa ,wengine wanapotea na sababu hazijirithishi na moja ya sababu inayopeleka twiga kuuawa kwa wingi ni sababu za kibiashara “
Alizitaja sababu zilizobaini twiga hao kuuwa ni kuwa mafuta yake ni dawa yanatumika katika tiba mbalimbali na pia sababu za kibiashara na kwasababu twiga ni mnyama mpole nyama yake ni nyingi ndio maana wanauwawa.
Alisema kamati imepata tarifa ya watu 25 wanaojihusisha na ujangili wilayani Longido na ametoa maelekezo watuhumiwa hao waliohusika na ujangili wakamatwe na hadi jana watuhumiwa watano wamekamatwa na wengine wamekimbilia nchi jirani ya Kenya.
“naagiza vyombo vya usalama viwakamate na nitaunda timu nyingine ili kuwahoji watuhumiwa hao waliokamatwa wahojiwe ili tupate tarifa za kina zitakazotuwezesha kupata taarifa kamili na kuaanda majalada vyema”
Pia kamati imebaini uzembe kwa baadhi ya wawekezaji ikiwemo kampuni ya Greenmills kwa kutokuwa na ushirikiano na wananchi na naagiza hao wamiliki wa vitalu vya uwindaji wilayani Longido wafike katika tume hii niliyounda kwa aajili ya kupata ufafanuzi zaidi na timu hiyo inawashirikisha usalama wa Taifa ,Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ),Polisi , taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na Mwakilishi kutoka Ofisi ya Mkuu wa MKoa.
“Wamiliki wa vitalu nitawataka waje katika kamati hii ili wahojiwe na huu ni wito wangu wa mwisho ili kubaini ni kwanini hawatoi fedha kwa vijiji walivyoingia navyo mikataba nasi tushauri serikali vitu vya kufanya”
Pia kamati imegundua Polisi Wilaya ya Longido hawatoi ushirikiano katika vita vya ujangili wilayani Longido ikiwemo kituo kidogo cha polisi cha Namanga ambacho kipo mpakani.
Na kusisitiza kuwa atamjulisha Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Simon Sirro pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani ,Kangi Lugola kumchukuliwa hatua OCD wa Wilaya ya Longido, Joshuani Kaijanante kwa kitendo chake cha kuidharau kamati aliyounda pamoja na kuzembea katika vita vya ujangili.
Pia wanamuomba mwansheria wa Mkoa wa Arusha kuongeza uelewa wake wa kisheria ili kuhakikisha majalada 27 ya ujangili yanapatiwa ufumbuzi sambamba na kesi kuendelea mahakamani badala ya kuahirishwa mara kwa mara.
Pia aliagiza Afisa Wanyamapori wilaya ya Longido,bwana Kubingwa kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo.
Gambo amemwomba Waziri wa maliasili na Utalii kuunda tume ya uchunguzi dhidi ya kampuni ya Green milles kutokana na kukiuka mikataba ya vijiji husika katika kuleta
Ofisi ya Tawa na Maliasili iratibu na kuendesha mafunzo ya uendeshaji wa mashauri hayo na uandishi wake ili kuwezesha kesi kushinda mahakamani ikiwemo Afisa wanyamapori Longido kuchukuliwa hatua zinazostahili
Naye Kaimu Kamishna wa Polisi Mkoa ,Longinus Tibishbwamu alikiri kukamata watuhumiwa watano kutokana na ujangili huo na kusisitiza kuwachukuliwa hatua wale wote wanaohusika na tuhuma hizo za ujangili na kwa wale waliokimbilia nchini Kenya alisisistiza jeshi hilo linaitelejensia ya hali ya juu katika kuwabaini na kuwakamata wahalifu wote waliohusika na ujangili wa wanyama hao.
Naye Mkuu wa wilaya ya Longido, Frank Mwaisumbe alimshukuru Rc Gambo kwa kuhakikisha tume hiyo imebaini mauji ya wanyama hao na kusisitiza kuwa wilaya hiyo inategemea sana uwindaji na ufugaji ingawa tume ilikumbana na vikwazo vingi lakini imekuja na majibu hayo ya ujangilli.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.