• Complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Arusha Regional

The United Republic of Tanzania President Office Regional Administration and Local Government Arusha Regional

  • Home
  • About Us
    • History
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa mikoa waliopita-Arusha
    • Dira na dhima
    • The basics
    • Strategies
  • Administration
    • Structure
    • Departments
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Units
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • District
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Councils
    • Arusha CC
    • Arusha DC
    • Meru DC
    • Monduli DC
    • Karatu DC
    • Longido DC
    • Ngorongoro DC
  • Investment Opportunities
    • Tourism
    • Livestock
    • Agricultre
    • Industrial
  • Our Service
    • Health
    • Education
    • Water
    • Land
    • Tourism
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events

UBADHILIFU WA  MILIONI 428 KUWAFIKISHA KIZIMBANI WATUMISHI ARUSHA..

Posted on: April 29th, 2024

Na Elinipa Lupembe

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda ameagiza kupandishwa kizimbani, watendaji wa Mkoa wa Arusha waliohusika na ubadhilifu wa shilingi milioni 428 fedha zilizotengwa kutekeleza mradi kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini, mradi unaotekelezwa na Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii - TASAF.

Mhe. Makonda ametoa agizo hilo, mara baada ya kujiridhisha na taarifa ya uchunguzi uliokuwa na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Arusha na kuona zipo sababu za Watendaji wote waliohusika kupandishwa kizimbani ili sheria iweze kuchukia mkondo wake.

Aidha, Mkuu wa Mkoa huyo, amekemea tabia ya  Watendaji wabadhirifu wanaoihujumu Serikali kwa kuiba fedha za Umma na kusisitiza kuwa, hatofumbia macho mtumishi ama kiongozi yoyote atakayekwenda kinyume na maadili ya Utumishi wa Umma, ikiwemo wizi wa mali za Umma.

"Ninatoa onyo kwa watumishi wote wa Umma, viongozi wa Chama na Serikali pamoja na wananchi wote wa mkoa wa Arusha, kujihadhari na vitendo vya rushwa kwa kuwa ni kinyume cha maadili ya Utumishi wa Umma na neno la Mungu, sitaweza kumkosea Mungu wala Kiongozi aliyeniteua Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ajli ya watu ambao sio waaminifu, wanaoweka mbele maslahi yao badala ya maslahi ya watanzania hususani wananchi wenye kipato duni" Amebainisha Mhe.Makonda

Hata hivyo, Mhe. Makonda ameiagiza Kamanda wa  TAKUKURU Mkoa huo, kufanya uchunguzi kwenye miradi yote saba iliyotekelzwa kupitia programu ya TASAF mkoa wa Arusha yenye thamani ya shilingi Bilioni 1.7, ili  kujiridhisha na taratibu zilizotumika pamoja na ubora wa miradi hiyo kwa kulinganisha na thamani ya fedha zilizotumika.

Amesisitiza pia kufanyika uchunguzi maalum kuhusu matumizi ya fedha zinazotolewa na serikali kwaajili ya Utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Arusha na kuahidi kuchukuliwa kwa hatua za kisheria kwa wote watakaobainika kujihusisha na wizi na matumizi mabaya ya fedha za maendeleo.

Ikumbukwe kuwa, Mhe. Makonda amefanya uchunguzi wa ubadhilifu wa fedha hizo,kufuatia malalamiko ya mwananchi kupitia video iliyozagaa kwenye mitandao ya kijamii kudhulumiwa fedha.

Announcements

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • View All

Latest News

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • View All

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
More Videos

Quick Links

  • Guildlines Towards the use of ICT In Government
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Public Servant Portal
  • Takwimu
  • TANAPA

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

Other Contacts

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Sitemap
    • FAQ

Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.