Waziri wa nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI ) Mhe. Mohamed Mchengerwa ameutangazia Umma wa Tanzania na Vyama vya siasa kuwa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Tanzania Bara utafanyika tarehe 27 November 2024
Waziri Mchengerwa ameeleza hayo leo tarehe 15 Agosti 2024 wakati akitoa Tangazo la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kuzindua nembo rasmi ya uchagunzi wenye kaulimbiu isemayo “ Serikali za Mitaa, Sauti ya Wananchi, Jitokeze kushiriki “.
“Ninautangazia Umma wa Watanzania na Vyama vyote vya Siasa vyenye Usajiri wa kudumu kuwa tarehe 27 Novemba 2024 itakuwa siku ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Tanzania Bara, Upigaji wa kura utaanza saa mbili kamili za Hasubuhi nakukamilika saa kumi kamili za jioni”
Waziri Mchengerwa amesema kuwa Kampeni zitafanyika siku saba kabla ya Uchaguzi na kampeni za uchaguzi zitafanyika siku saba kabla ya uchaguzi na kubainisha kuwa kila chama cha siasa kinachoshiriki uchaguzi kitawasilisha ratiba yake ya mikutano ya kampeni ya uchaguzi kwa Msimamizi wa Uchaguzi si chini ya siku saba kabla ya kuanza kampeni .
Aidha, Mchengerwa amebainisha kuwa majina na mipaka ya vitongoji yatangazwe siku 72 kabla ya uchaguzi kwa mujibu wa kanuni na kufahamisha Wananchi, majina ya maeneo na mipaka ambayo itahusika katika kujiandikisha na upigaji wa kura ambapo Wasimamizi wa Uchaguzi watatangaza majina na mipaka ya vitongoji vilivyoko katika eneo la Halmashauri husika .
Kadhalika , Waziri Mchengerwa ametoa wito kwa Wananchi kujitokeza kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa kwa kugombea na kuchagua Viongozi .
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.