Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda amekutana na kufanya Mazungumzo na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima ofisini kwake mapema leo Mei 2, 2024.
Katika Mazungumzo yao, Mhe. Waziri Gwajima amempongeza Mhe. Makonda kwa kuendelea kuyatambua na kuyawezesha makundi mbalimbali ya kijamii ikiwemo kundi la Vijana maarufu kama 'Wadudu' linalojishughulisha na shughuli mbalimbali za sanaa mkoani Arusha.
Mhe. Gwajima miongoni mwa Mawaziri, waliohudhuria sherehe za Mei Mosi kwenye Viwanja vya Sheikh Amri Abeid mjini Arusha na leo amekutana na Menejimenti ya Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.