Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Paschal Katambi (Mb) amefika kwenye Ofisi ya Mkuu wa Arusha na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Paul Christian Makonda mapema leo Aprili 20, 2024
Mhe. Katambi yuko mkoani Arusha kwa ajili ya maandalizi ya Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi inayofanyika Kitaifa Mkoani Arusha.
Naibu Waziri Katambi amepata wasaa wa kuzungumza na Viongozi wa Kamati ya Maandaliz ya Mei Mosi maandalizi ambayoa yanaendelea vizuri
Hata hivyo, Mhe. Katambi baada ya kupokea taarifa za Kamati zote, amewapongeza wajulbe wote kwa kazi nzuri waliyoifanya kwa ajili ya Maandalizi ya Mei Mosi na kuwataka kuendelea kushikamana mpaka kilele cha Sherehe hizo Mei 01, 2024.
Awali, Mei Mosi Kitaifa inafanyika Mkoani Arusha na Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.