Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe Dkt. Hussen Ali Mwinyi, amewasili mkoani Arusha na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda, Viongozi wa Chama na Kamati ya Usalama Mkoa kwenye Kiwanja cha Ndege cha Arusha, jioni ya leo Mei 16, 2024.
Rais Mwinyi amefika mkoani Arusha kwa ajili ya kufungua Semina ya WanaHisa wa Benki ya CRDB Tanzania, inayotarajiwa kufanyika kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC), mkoani Arusha mapema Mei 17, 2024.
Semina hiyo yenye Kauli Mbiu ya 'Ukuaji wa Pamoja' itafuatiwa na Mkutano Mkuu wa 19 wa Wanahisa wa Benki hiyo ya CRDB Mei 18, 2024 huku lengo la mkutano huo likiwa ni kujadili kilichofanyika kwa kipindi cha mwaka mmoja, kujadili utekelezaji wa mkakati wa Utendaji kwa kipindi cha miaka mitano 2023 - mpaka 2027 pamoja na kuweka mipango kwa miaka ijayo.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.