Na Elinipa Lupembe.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa @kassim_m_majaliwa amewasili Mkoani Arusha na kupokelewa na Mkuu wa wilaya ya Monduli Mhe. Festo Kiswaga na viongozi wengine wa Chama na Serikali, kwenye uwanja wa Ndege Arusha kwa ndege ya shirika la Ndege Tanzania, mapema leo Novemba 04, 2024.
Mhe. Majaliwa yupo Mkoani Arusha akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan @samia_suluhu_hassan, katika Ufunguzi wa Mkutano wa 9 wa Mtandao wa Mameneja na Wasimamizi wa Rasilimali Watu katika sekta za Umma Barani Afrika 2024, unaofanyika mkoani Arusha kwenye Kituo cha Mikutano ya Kimataifa Arusha (AICC) kuanzia tarehe 04 - 07, Novemba, 2024.
Kauli mbiu ya mkutano huo ni "Utawala Stahimilivu na Ubunifu; Kutunza Sekta ya Umma Ijayo Kupitia Uongozi wa Rasilimali Watu"
@owm_tz @ikulu_mawasiliano @ofisiyarais_utumishi2019 @tume_utumishiwaumma @utumishiportals @ortamisemi @owm_tz
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.