Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Pindi Chana @pindi.chana amefika kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha na kupokelewa na Katibu Tawala Mkoa, Missaile Albano Musa asubuhi ya leo Mei 2, 2024.
Mhe. Balozi Chana licha ya kusaini kitabu cha wageni amefanya mazungumzo mafupi na Katibu Tawala ambapo ameleeza kuwa yuko mkoani Arusha kwa ziara ya kikazi ambapo atatembelea Mahakama za Kimataifa zilizopo mkoani Arusha
Aidha amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Paul Chritian Makonda kwa kazi kubwa anayoifanya ya kushughulikia kero za wananchi hususani kukusanya kundi la vijana na kuwawezesha kujipatia kipato kwa njia halali na kuepuka kujiingiza kwenye vitendo vya uhalifu.
"Tunampongeza Mhe. Makonda kwa kukutana na kundi la wadudu, kundi ambalo ameahidi kuliwezesha kufanya shughuli halali za kujiingizia kipato kwa kuzingatia kuwa, tunaye Mkurugenzi wa Mashitaka anayeshughulikia makosa ya jinai, ambapo vijana ni wateja wetu, hatupendi kundi la vijana kuwepo kwenye makosa hayo, tunapompongeza sana kwa jihata anazozichukua kwa vijana, ili wawe bizy kwenye kazi za kujenga Taifa". Amebainisha Mhe. Chana
Hata hivyo, Katibu Tawala huyo, amemkaribisha Mhe. Chana na kuahidi kumpa ushirikiano muda wote awapo mkoani Arusha, huku akifafanua kuwa, licha ya Mkuu wa Mkoa kukutana na kulitangaza kundi hilo la vijana, Ofisi yake imepanga kuwakutanisha vijana hao na watalamu wa fani mbalimbali ili kuwajengea uwezo wa kufanya kazi kupitia rasilimali zilizopo na zaidi kuwawezesha kunufaika na sekta ya utalii.
Awali, Mhe. Chana yuko mkoa Arusha kwa ziara ya kikazi ya kutembelea Mahakama ya Afrika na Haki za Binadamu na Watu pamoja na Mahaka ya Afrika Mashariki.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.