• Complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Arusha Regional

The United Republic of Tanzania President Office Regional Administration and Local Government Arusha Regional

  • Home
  • About Us
    • History
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa mikoa waliopita-Arusha
    • Dira na dhima
    • The basics
    • Strategies
  • Administration
    • Structure
    • Departments
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Units
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • District
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Councils
    • Arusha CC
    • Arusha DC
    • Meru DC
    • Monduli DC
    • Karatu DC
    • Longido DC
    • Ngorongoro DC
  • Investment Opportunities
    • Tourism
    • Livestock
    • Agricultre
    • Industrial
  • Our Service
    • Health
    • Education
    • Water
    • Land
    • Tourism
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events

UGONJWA WA VIKOPE KUWA TISHIO

Posted on: October 5th, 2018

Viongozi wa Wilaya wa Mkoa wa Arusha wametakiwa kusimamia kikamilifu zoezi la utoaji dawa za ugonjwa wa vikope (Trakoma) kwenye maeneo yao kwa lengo la kuhakikisha ugonjwa huu unatokomezwa kabisa.

Akitoa rai hiyo alipokuwa akifungua semina ya mpango wa kudhibiti magonjwa yasiyopewa kipaombele  kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, katibu tawala wa mkoa Richard Kwitega amesema ni vizuri viongozi wakajikita kwa nguvu zote katika zoezi hili lakutokomeza ugonjwa wa vikope kwenye maeneo yao.

“Ni rai yangu kwenu viongozi wote wa Wilaya na halmashauri kuhakikisha mnasimamia vyema zoezi hili lakutokomeza ugonjwa huu wa vikope katika maeneo yenu”.

Lengo la serikali nikutumia rasilimali chache kuthibiti magonjwa haya ambayo yanaonekana hayapewi kipaombele katika jamii yetu hivyo kila halmshauri ihakikishe inatenga fedha zakutosha zakusaidia upasuaji wa vikope.

Wilaya ya Karatu na halmashauri ya Arusha zimejitaidi kuhakikisha zimetokomeza ugonjwa wa vikope lakini bado katika halmashauri ya wilaya ya Longido na Ngorongoro, nguvu zaidi zinaitajika katika maeneo haya.

Kwa mkoa wa Arusha watu takribani 1076 wameshafanyiwa upasuaji wa vikope katika halmshauri zote za wilaya na magonjwa yanayoongoza katika mkoa huu ni ugonjwa wa Kichocho ,Minyoo ya Tumbo na vikope.

Amewataka washiriki wa semina hiyo kuhakikisha kuwa elimu wanayoipata katika mafunzo hayo wakaitumie vizuri katika kutokomeza magonjwa hayo kwenye maeneo yao.

Nae mratibu wa magonjwa yalisiyopewa kipaombele  kutoka Wizara ya Afya, maendeleo ya jamii,jinsia, wazee na watoto Dokta Upendo Mwingira, amesema takribani magonjwa 17 yasiyopewa kipaombele yapo katika bara la Asia, Amerika ya Kusini na Kusini mwa jangwa la Sahara.

Amesema magonjwa mengine ambayo hayapewi kipaombele ni AIDS, TB, Malaria, Kuumwa na nyoka,Matende, Mabusha, Usubi na Ukoma.

Amezitaja athari mbalimbali zinazotokana na magonjwa haya ni kama mgonjwa kupata ulemavu wa mda mrefu, Udumavu kwa watoto,kupunguza uwezo wa kufanya kazi,unyanyapaaji, kansa ya kibofu cha mkojo, upofu na presha ya ini.

Akitoa taarifa fupi ya ugonjwa wa vikope kwa mkoa wa Arusha Dokta Mwanahawa Kombo kutoka hospitali ya Mkoa Mt. Meru, amesema jumla ya wagonjwa 1076 wameshapasuliwa vikope na halmashauri ya Monduli imefanya vizuri katika kukabiliana na ugonjwa huu kati ya halmashauri 2 za Longido na Ngorongoro.

Semina hii hufanyika kila mwaka kwa lengo la kutoa elimu na takwimu sahihi za hali  halisi ya magonjwa yasiyopewa kipaombele nchini.

Announcements

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • View All

Latest News

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • View All

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
More Videos

Quick Links

  • Guildlines Towards the use of ICT In Government
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Public Servant Portal
  • Takwimu
  • TANAPA

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

Other Contacts

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Sitemap
    • FAQ

Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.