Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mheshimiwa Idd Hassan Kimanta, amemuagiza Mkurugenzi wa jiji la Arusha bwana Daktari Marco Pima kutohamisha mpango wa ujenzi wa Kanisa Katoriki la Parokia ya Sinoni.
Kimanta ameyasema hayo alipotembelea eneo hilo la ujenzi wa Kanisa uliositishwa kutokana na kujenga karibu na shule ya sekondari Terrat katika halmashauri ya jiji la Arusha.
Amesema eneo hilo nila Kanisa lenye ukubwa wa mita za mraba 7873 hivyo wasiingiliwe katika mipango yao ya ujenzi, ila kama wataalamu wa Jiji watataka kushauri wasubiri uongozi wa Kanisa hilo wakileta maombi ya ujenzi ndio wawashauri namna ya kujenga.
Pia, amesema hata mpango wa kubadilisha eneo hautakiwi kwakuwa eneo hilo ni mali ya Kanisa na uendelee kuwa mali ya Kanisa.
Amesisitiza kuwa maamuzi hayo yametolewa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuli ya Muungano wa Tanzania Daktari John Pombe Magufuli na yeye kama msaidizi wake ameagiza yatekelezwe.
Akitoa neno la shukrani kwa Mheshimiwa Rais Katekista wa Kanisa hilo bwana Filipo Jakobo, amesema wanamshukuru sana Rais kwa uamuzi huo wa kuwaachia eneo lao na kuendelea na ujenzi wa kanisa hilo.
Mkuu wa Mkoa ametembelea eneo hilo ikiwa na moja ya maeneo ya ziara yake aliyoifanya katika jiji la Arusha.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.