Na Elinipa Lupembe.
Ujumbe wa Mabalozi kutoka, Umoja wa Nchi za Jumuiya ya Ulaya, wakiwa kwenye mkutano mfupi, na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. John V.K Mongelwa, uliofanyika kwenye Ukumbi wa mikutano ofisi ya mkuu wa mkoa huo.
Mabalozi hao wamefika mkoani Arkika, kwa ajili kufanya kikao na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Chama cha Waendeshaji Watalii Tanzania (TATO) pamoja na kutembelea Hospitali ya Lutheran Arusha (ALMC), jijini Arusha, pamoja na shughuli nyingine za kijamii.
Awali, Mhe. Mongella ametumia fursa hiyo, kuwakaribisha mkoani Arusha, na kuwaelezea kuwa, Serikali ya Tanzania inatambua na kuthamini ushirikiano na mchango wa Nchi za Umoja za Jumuya ya Ulaya kwenye sekta ya kijamii na kiuchumi.
Licha ya kuwakaribisha, Mabalozi hao Mkoani Arusha, Mhe. Mongella amewahakikishia hali ya usalama muda wote watakaokuwa Arusha, na yuko tayari kutoa ushirikiano muda wate watakapohitaji msaada.
"Nichukue fursa hii, kuwakaribisha Arusha, mkoa huu unazo fursa nyingi za uwekezaji, katika sekta ya Utalii na Kilimo, ninategemea mtafurahia hali ya hewa nzuri ya Arusha, pamoja na vivutio vya utalii vinavyopatikana mkoani kwetu" Amesema
Naye Kiongozi wa Mabalozi hao, ambaye ni Mkuu wa Utawala, Umoja wa Nchi za Ulaya Nchini Tanzania, Loic de Bastier, amemshukuru mkuu wa mkoa huyo,
kwa niaba ya wenzake, kwa namna alivyo wakarimu mara walipofika ofisini kwake, na kuahidi kuendelea kuimarisha Uhusiano wa Kidiplomasia kati ya Tanzania na Nchi za Umoja wa Jumuiya ya Ulaya.
Mabalozi hao watafanya shughuli zao, mkoani Arusha kwa siku mbili 23- 24 .11.2023, pamoja na shughuli nyingine, watashiriki mikutano, itakayofanyika kwenye Hotel ya Gran Mellia ya Jijini Arusha.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.