"Nendeni mkatunze mazingira na vyanzo vya maji ili yasiendelee kutuadhiri katika maisha yetu".
Yamesemwa hayo na Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongella alipokuwa akishiriki zoezi la kupanda miti katika shule ya Sekondari Meserani Wilayani Monduli.
"Upandaji miti kunasaidia kutunza mazingira na kupunguza ukame".
Amewataka wananchi kusimamia maelekezo yanayotolewa na viongozi wa Serikali hasa kupanda Miti katika makazi yao, mashamba, Shule, Makanisani na Misikitini.
Mazingira ni uhai wetu tunapoyaharibu yanatugharimu haraka sana ikiwemo kukosa mvua kwa wakati na Mifugo kufa.
Mkuu wa Wilaya ya Monduli Sulemani Mwenda amesema ataenda kusimamia maelekezo yaliyotolewa na RC Mongella akiwemo kwenda kukagua miti yote iliyopandwa ili ajiridhishe.
Pia, ataenda kuwasimamia wakuu wa idara katika maeneo waliyopangiwa kuyasimamia wanayasimamia hasa katika kupanda miti katika vyanzo vya Maji.
Amesema, katika Wilaya yake atahakikisha taasisi zote zinapanda miti na wanafunzi wanakuwa na Miti yakuitunza katika shule zao.
RC Mongella, amezindua zoezi la upandaji Miti Katika Wilaya ya Monduli ikiwa ni moja ya maelekezo yake ya kila halmashauri kuhakikisha inapanda Miti 1,500,000 kwa mwaka 2022/2023 na halmashauri hiyo imeshapanda miti 1,517,223.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.