Umati wa watu waliojitokeza kushuhudia mashindano ya pikipiki ya Samia Motocross Championship kwenye viwanja vya Laki laki Kisongo Jijini Arusha leo Julai 14, 2024.
Mashindano hayo yatakayokoma jioni ya leo, mshindi wa kwanza atazawadiwa fedha taslimu shilingi Milioni 10, mshindi wa pili Milioni 7 na mshindi wa tatu atazawadiwa Milioni 5 huku washiriki wengine wakizawadia zawadi mbalimbali.
Kulingana na Muasisi wa mashindano hayo Mhe. Paul Christian Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, washindi wa tatu wa juu wa mashindano hayo watawezeshwa kushiriki kwenye mashindano ya kimataifa ikiwemo ya Nchini Morocco yanayotarajiwa kufanyika mwezi Septemba mwaka huu.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.