Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka viongozi walioteuliwa ni kama ifuatavyo:-
i. Prof. Harun Jeremia Mapesa ameteuliwa kuwa Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere. Kabla ya uteuzi huu, Prof. Mapesa alikuwa Mhadhiri Mwandamizi Chuo Kikuu cha Mzumbe, anachukua nafasi ya Prof. Shadrack Mwakalila ambaye amemaliza muda wake , na
ii. Mhandisi Peter Rudolf Ulanga ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL). Mhandisi Ulanga anachukua nafasi ya Mhandisi Ladislaus Matindi ambaye amestaafu.
Uteuzi huu umeanza tarehe 09 Novemba, 2024.
Imetolewa na Sharifa B. Nyanga
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.