Ushirikishwaji katika kutoa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi kutoka katika sekta mbalimbali hasa za dini,kisiasa na kabila ni muhimu sana.
Akiyasema hayo kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro amesema kuwa zoezi hili lisichanganywe na mambo ya siasa bali sekta hizo zitumike kutoa elimu zaidi.
Ameyasema hayo alipokuwa akizindua utoaji wa chanjo hiyo kimkoa katika shule ya msingi Ngarenaro,ambapo amesema wasichana 21,198 watapatiwa chanjo hiyo kwa mkoa wa Arusha.
Aidha,saratani ya mlango wa kizazi niya pili baada ya saratani ya matati, kwa asilimia 38 na niya kwanza kwakuwa na vifo vingi kwa Tanzania, ikifuatiwa na saratani ya shingo ya kizazi kwa asilimia 32.8,saratani ya koo asilimia 10.9 na saratani ya tezi dume kwa asilimia 2.1.
Chanjo hii inapatikana katika vituo vyote vya afya na ni bure kwa wasichana wenye umri wa miaka 14.Kila mwaka wanawake 466,000 wanathibitika kuwa na saratani ya mlango wa kizazi.
Akizungumza kwa niaba ya katibu tawala wa mkoa wa Arusha,mganga mkuu wa mkoa wa Arusha Vivia Tomothy Wonanji, amesema kila mtoto aliyefikisha miaka 14 anatakiwa kupatiwa chanjo hii na itarudiwa baada ya miezi sita ya chanjo ya kwanza.
Amewashukuru wadau wote walioshirikiana na Serikali katika kufanikisha upatikanaji wa chanjo hii na bure nchi nzima.
Amewatoa shaka wananchi wote kuwa chanjo hiyo ni salama kabisa na elimu itaendelea kutolewa kwa watu ili kuwaondoa wasiwasi wakuwa chanjo hii inaharibu kizazi.
Chanjo hii yakuzuia saratani ya mlango wa kizazi ilizunduliwa hivi karibuni nchini na waziri wa afya,maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Ummi Mwalimu na kufuatia uzinduzi mdogo katika mikoa na halmashauri zote ambapo kwa Arusha ilizinduliwa mnamo Aprili 25,2018.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.