Vijana wa Kujitolewa isaidieni serikali kuhamasisha wananchi wajiunge na mfuko wa jamii wa bima ya afya (CHF) ili kuwasaidia wananchi waweze kupata matibabu bora na kujenga afya zao.
Ameyazungumza hayo katibu tawala wa Mkoa wa Arusha bwana Richard Kwitega alipokuwa akifunga maadhimisho ya kimataifa ya siku ya kujitolea,katika wilaya ya Arumeru.
Amesema ni jukumu la kila mmoja kuwa tayari kujitolea katika nyanja mbalimbali ili kuleta maendeleo kwa mtu binafsi na jamii kwa ujumla.
Mkurugenzi wa halmshauri ya Meru ndugu Emmanuel Mkongo, amesema, serikali pia haipo nyuma katika kuhakikisha dhana kamili ya kujitolewa inatekelezwa kwa umakini zaidi kwa kuyapa kipaombele zaidi malengo endelevu ya dunia (sustainable development goals SDG’s) katika nyanja zote za maendeleo.
Ameshauri mashirika yote na azaki kuendendelea kuwahamashisha vijana kufanya kazi za kujitolea zaidi hasa katika sekta ya afya hasa kwenye maeneo ya mazingira magumu.
Mwakilishi kutoka umoja wa mataifa (UN) bi. Christine Msisi amesema, dhana ya kujitolea ni muhimu sana kwa kijana kwani inamsaidia kufikisha malengo yake na pia husaidia kujenga mahusiano na watu mbalimbali.
Amesema umoja wa mataifa unaendelea kuhamasisha vijana kujitolea katika nyanja mbalimbali kwani mpaka sasa ni vijana 65 tu wanajitolea katika mashirika mbalimbali.
Peter Owaga Mkurugenzi mtendaji wa shirika la DSW amesisitiza kuwa vijana wanaojitolea hujifunza mambo mengi ikiwemo maswala ya uongozi na ujasiliamali ambayo yamewasaidia sana kufikia malengo yao.
Siku ya kujitolea duniani huadhimishwa kila mwaka na mwaka huu kauli mbiu ilikuwa “kuwawezesha watu katika kuhakikisha na kuleta umoja na usawa”,ambapo vijana wanaojitolea kutoka mashirika mbalimbali duniani walishiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii kamavile kufanya usafi na kupanda miti katika halmashauri ya Meru.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.