Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Richard Kwitega amewataka vijana kusubiri kuajiriwa.
Ameyasema hayo alipokuwa akizindua mpango wa udhamini wa masomo kwa vijana kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, udhamini huo umetolewa na taasis ya GICCS kwa kushirikiana na chuo cha JR cha Jijini Arusha.
Kwitega amewataka vijana hao kutumia elimu yao kulijenga Taifa ambalo linakuwa kwa kasi kubwa sana na kuweza kupambana na umaskini.
Aidha, amesema kwa teknolojia mbalimbali zilizobuniwa na wanafunzi hao zisambazwe katika maeneo mbalimbali ili ziendelee kukua kwa kasi.
Taasis ya GICCS imedhamini jumla ya vijana 50 kwa ajili ya masomo ya TEHAMA na biashara kwa mwaka 2020 na mwaka 2019 walidhamini jumla ya vijana 14.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.