Vijana wanaokeshwa mikopo ya Serikali kupitia program za Uwezeshaji wananchi kiuchumi ikiwepo mikopo isiyokuwa na riba inayotolewa kupitia aslimia 10 za mapato, endapo watarejesha vizuri kwa uaminifu wapewe kipaumbele cha kukopeshwa tena.
Rai hiyo imetolewa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2024, Ndugu Godfrey Eliakimu Mnzava wakati alipotembelea mradi wa uwezeshaji wananchi kiuchumi kikundi cha Vijana cha Iloonyok, vijana wanaojishughulisha na ufugaji kwa kununua, kunenepesha na kuuza mifugo ng'ombe, mbuzi na kondoo, waliokopeshwa kiasi cha shilingi milioni 4 kupitia mapato ya ndani ya halmashauri ya Longido
Amewapongeza vijana hao, kwa kujiajiri kwa kazi nzuri inayowaingizia kipato na kukwamua uchumi wa familia na Taifa kwa ujumq wake.
Amemuagiza Mkuu wa wilaya ya Longido kuendelea kuwasimamia vijana ili waweze kukabiliana na changamoto ya ajira nchini na duniani kwa kujiajiri kupitia fursa za mikopo inayotolewa na Serikali.
"Niwatie moyo vijana wenzangu kwa kazi nzuri mnayoifanya kwa maendeleo ya Taifa lenu laTanzani, mmetumia fursa ya mikopo ya serikali na kurejesha kwa wakati, kumbukeni Taifa linawategeme vijana ambao ndio nguvukazi, lakini nishauri viongozi kuwapa kipaumbele vijana ambao wanakopeshwa na kurejesha mikopo kwa wakati.
Akiwasilisha taarifa ya mradi huo, Mwenyekiti wa Kikundi Looyan amsema kuwa mkopa wa milioni 4 umekuza mtaji wao na kufikia mifugo 30 na kufikia 40 huku wakiwa wamekamilisha marejesho yote ya mkopo huo.
Tukopeshwa shilingi milioni 4, tumeongeza idadi ya mifugo na faida tuliyoipata kila mwanachama alipata shilingi laki 3 kwa ajili ya kununua bati za kuezekea nyumba, tunaishi kwenye nyumba za bati" Amesema
Aidha ameishukur serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Dkt.Samia Suluhu Hassan kuwa na programu imara za uwezeshaji vijana kuinuka kiuchumi huku wakiweza kujiajiri jambo ambalo limewanufaisha vijana hadi wa maeneo ya vijijini, wameweza kujiajiri kupitia futsa zinazopatikana kwenye maeneo yao.
Kauli Mbiu ya Mwenge wa Uhuru 2024 ni "Tunza Mazingira, Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa ujenzi wa Taifa Endelevu"
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.