Na Elinipa Lupembe
Vikundi vya vijana wajasiriamali mkoani Arusha wameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kuweka mazingira rafiki yanayowapa fursa vijana kuwa wabunifu kupitia rasilimali rahisi zinazopatikana kwenye mazingira yao na kujiari pamoja na kuajiri vijana wenzao.
Vijana wayasema haya wakati wa maonesho ya Wiki ya vijana kitaifa, yaliyofanyika kwenye viwanja vya Stendi ya Zamani Babati mkoani Manyara yaliyohusisha ubunifu, utangazaji na uuzaji wa bidhaa zao.
Mwenyekiti wa kikundi cha
Grin Makers Solution Tz, kinachofanya shughuli zake, halmashauri ya Arusha wailaya ya Arumeru, Bartazari Ansen Twati amethibitisha kuwa baada ya kikundi hicho kuwa na wazo la kutengeza mashine za kufyatulia matofali watalamu wa serikali walipokea wazo hilo na kuwaunganisha na wadau wa sekta nyingine jambo ambalo limewawezesha kuwa na kiwanda kidogo cha kutengeneza 'paving blocks' za plastiki kwa kutumia taka za plastiki.
"Tulipoanzisha wazo letu, tulikuwa na hofu lakini serikali imetushika mkono kwa kuanza biashara na kufanya mchakato wa kusajili kiwanda chetu, kupata vibali vyote vya uzalishaji pamoja na kutuweka kwenye mchakato wa kupata mkopo kupitia Mfuko wa Vijana Ofisi wa Waziri Mkuu, tunategemea kupata mkopo mkubwa wa kuendesha na kuongeza uzalishaji katika kiwanda chetu" Amesema Twati.
"Tunamshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa fursa za sekta mbalimbali zilizofunguliwa kwa vijana wa kitanzania, ambazi zimewapa ujasiri vijana wengi kuthubu kujiajiri huku wengi wakipata mafanikio makubwa ya kichumi na kijamii"
Naye James Emmanuel Mwenyekiti wa kikundi cha Amani Barazani kinachojishughulisha na ukoji wa vitafunio wilayani Karatu, amesema kuwa kupitia mikopo isiyokuwa na riba inayotolea na halmashauri, wameweza kubadilisha biashara yao kutoka kupika maandazi na kununua mashine ya kuokea vitafunioa vya aina zote.
"Mwanzo hatukuamini kuhusu mikopo isiyokuwa na riba, tulidhani ni ubabaishaji tuu, lakini tulipewa elimu ya mikopo hiyo na hatimaye kukopeshwa shilingi milioni 8 fedha ambazo zimetuwezesha kununua 'oven' na mashine nyingine za kukandia unga" Ameweka wazi James
Sara Lazaro Mwenyekiti wa kikundi cha Emanyata Youth Group cha wilayani Longido wanaojihusisha na utengenzaji wa urembo kwa kutumia shanga, amesema kuwa zamani ilikiwa sio rahisi kuwa kabila la Kimaasai kuwakutanisha vijana wa kike na kiume kufanya kazi pamoja, serikali imefanya kazi kubwa sana ya kutoa elimu na kuwaunganisha vijana wa jinsi moja na sasa wanafanya kazi pamoja kama timu.
"Kila mtu alikuwa tunatengeza bidhaa zake mwenyewe kupitia serikali tumeweza kuungana na kupewa mkopo wa milioni 8, fedha ambazo licha ya kuonheza mitaji kwenye biasha zetu, umetuwezesha kununua mashine ya kusaga na kukoboa nafaka, kazi ambazo zimeweza kutuongezea vipato na kukuza uchumi wa familia kwa maendeleo ya Taifa letu" Amesema Sara
Hata hivyo Kaimu Afisa Vijana mkoa wa Arusha , Hanifa Ramadhani amesema kuwa serikali ya awamu ya sita inayo mikakati mingi kisekta ya kuwajengea uwezo vijana wa kujiajiri licha ya kuwa na programu tofauti za kuwapa mikopo ya kukuza mitaji zipo programu nyingine za kuwapa elimu ya kujiajiri, kufanya biashara, kuweka na kukopa, kukuza mitaji, kupata vibali vya biashara zao ikiwa ni pamoja na kusajili vikundi, kusajili biashara, kulipa ushuru, kodi na tozo za serikali kwa kuwaunganisha kwenye Mamlaka husika.
"Serikali inawasimamia vijana kuweza kujiajiri kwa kiwapa mikopo siyokuwa na riba inayotolewa na halmashauri, upo Mfuko wa Ofisi ya Waziri Mkuu, programnya Kilimo BBT, imasimamiwa na wizara ya Kilimo,program za Jeshi la Kujenga Taifa zote zina lengo la iwajengea uwezo wa kujitegemea katika kulitumikia Taifa la Tanzania" Amefafanua Afisa Vijana huyo
Maonesho ya wiki ya Vijana Kitaifa yamehitimishwa leo ikiwa ni kumbukizi ya Kifo cha Hayati Baba wa Taifa Mw. Julius Kambarage Nyerere na Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 yenye Kauli mbiu ya Vijana na Ujuzi Rafiki wa Mazingira kwa Maendeleo Endelevu.
#Arushafursalukuki
#kaziinaendelea
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.