Viongozi wa Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini ( TGCO), wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa TGCO Taifa, Abdul Njaidi, wamefika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa huo Mhe. John V.K Mongella leo Februari 26, 2024.
Viongozi hao, licha ya kusaini kitabu cha wageni wamemueleza Mkuu wa mkoa kuwa, wapo mkoani Arusha kwa ajili ya Mkutano Mkuu wa Chama hicho ambao unategemea kuwa na washiriki takribani 400, mkutano utakaofanyika kwenye Kituo cha Mikutano ya Kimataifa Arusha (AICC) Kuanzia tarehe 27 - 29 Februari, 2024.
Hata hivyo Mhe.Mongella amewakaribisha mkoani Arusha na kuwahahikisha kuwa Arusha ni salama na watapata ushirikiano wa kutosha, wakati wote watakapokuwa Arusha pamoja na kufurahia mandhari na hali ya hewa nzuri ya Jijini Arusha.
Aidha amewapongeza kwa kuichagua Arusha, kufanya mkutano wa TAGCO wa Mwaka na kufafanua kuwa Serikali inatambua mchango mkubwa unaotolewa na wanataaluma hao kwa kuwahabarisha wananchi shughuli zinazofanywa na Serikali, ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa shughuli na miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.