Balaza linatakiwa kuwa na Umoja, Mshikamano na kauli moja katika maamuzi ya kuleta maendeleo kwa wananchi
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella alipokuwa akizungumza kwenye kikao cha kujadili hoja za mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali cha Jiji la Arusha.
Amesema kuwa na kauli moja kwa viongozi kunasaidia sana kuepusha migogoro, inaleta maendeleo na amani kwa wananchi.
Aidha, amesema mabalaza yanatakiwa kuwa ya wazi na kweli ili kutatua changamoto kwa haraka.
Pia,amewataka madiwani hao kufanya kazi kwa uwadilifu, uzalendo na wawe wachapa kazi kwani Jiji la Arusha ndio kioo cha Mkoa mzima.
Nae, Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Dkt. Athman Kihamia amesema ofisi ya Mkoa itashirikiana kwa ukaribu na Jiji la Arusha ili kuleta maendeleo kwa pamoja.
Dkt. Kihamia ameitaka ofisi inayofunga mahesabu kushirikiana na ofisi ya mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za Serikali ili kuepusha makosa madogo madogo ambayo yamejitokeza kwa mwaka wa fedha 2019/2020.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Kenan Kihongosi amewataka watumishi hao kufanya kazi kwa kufuata Sheria na miongozo ya serikali ili kuondoa migongano.
Pia, amemtaka Mkurugenzi wa Jiji la Arusha kuendelea kukusanya mapato zaidi ili fedha hizo zikatumike katika kuleta maendeleo ya Jiji hilo.
Viongozi hao walihudhuria kikao hicho cha kujadili hoja za mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali cha Jiji la Arusha.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.