Wajumbe wa Kamati ya Biashara,Fedha na Uhamiaji kutoka Bunge la Afrika wameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuhakikisha inaondoa vikwazo vya kibiashara kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) katika kufikia eneo la Biashara Huru Bara la Afrika (AfCFTA) .
Pongezi hizo zimetolewa na wajumbe wa kamati hiyo wakiongozwa na Pro. Magret Kamar ambaye ni kiongozi wa ujumbe wa bunge la hilo wakati walipotembelea Kituo cha Huduma za Pamoja Mpakani (OSBP) eneo la Namanga wilayani Longido Mkoani Arusha
Pro. Kamar amesema katika ziara hiyo wamefika nchini Tanzania kujionea utaoji wa huduma katika maeneo mbalimbali ya mipakani na kwa upande wa mpaka wa Namanga wamejionea jinsi nchi ya Tanzania inavyojitahidi kuhakikisha suala la usalama mipakani linaimarika ikiwemo utoaji na uingizwaji wa mizigo kupitia mashine za kisasa za ukaguzi.
Amesema kuwa ajenda kubwa ya mabunge hayo ni kuhakikisha biashara Huru zinaimarika maeneo ya mipakani na wamejionea kwa macho yao juu ya biashara hizo na hatua zinazostahili katika ukaguzi mzuri unaofanywa katika eneo hilo la mpaka wa Namanga
"Tumekuja kujionea jinsi gani nchi ya Tanzania inavyotekeleza fursa za biashara na jinsi ambavyo bidhaa zinazotokea nchi za EAC ikiwemo udhibiti wa bidhaa na uingizwaji lakini pia eneo la biashara huru lipoje tumeridhika na utaoji huduma nzuri katika maeneo ya mipaka hususani mpaka huu wa Namanga unao unganisha nchi ya Kenya na nchi zingine "
Naye Mbunge kutoka Bunge la Shelisheli ,Wavel Woodcock amesema ujumbe huo umeridhishwa na utoaji huduma bora maeneo ya mpakani na serikali ya Tanzania imejitahidi katika sekta ya miundombinu ikiwemo maeneo ya mipakani na eneo la biashara katika nchi za EAC kukua zaidi na kuinua uchumi wa kila mwananchi.
Hata hivyo ameziomba nchi za Afrika kuhakikisha wanajadili changamoto walizonazo na kuzitatua ili kuhakikisha usalama unaimarika pamoja na uchumi kwa wafanyabiashara, wananchi husika na nchi kwa ujumla katika kuleta maendeleo.
Naye Mbunge wa Viti Maalum ,Anatropia Theonest amesema mafanikio ni mengi kwa upande wa Tanzania lakini pia wamesikia maelezo kutoka kwa wahusika wa mipakani ikiwemo uharakishwaji wa utoaji mizigo inayoingia na kup
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.