• Complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Arusha Regional

The United Republic of Tanzania President Office Regional Administration and Local Government Arusha Regional

  • Home
  • About Us
    • History
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa mikoa waliopita-Arusha
    • Dira na dhima
    • The basics
    • Strategies
  • Administration
    • Structure
    • Departments
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Units
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • District
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Councils
    • Arusha CC
    • Arusha DC
    • Meru DC
    • Monduli DC
    • Karatu DC
    • Longido DC
    • Ngorongoro DC
  • Investment Opportunities
    • Tourism
    • Livestock
    • Agricultre
    • Industrial
  • Our Service
    • Health
    • Education
    • Water
    • Land
    • Tourism
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events

WACHEZAJI WA ZAMANI WAKUMBUKWE-RC KIMANTA

Posted on: May 7th, 2021


Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Iddi Hassan Kimanta amekabidhi kiasi cha shilingi Milioni 11 kwa vituo vya kulelea watoto yatima na kwa Bw.  Allan Shomari,  mchezaji wa zamani wa mpira wa miguu  aliyewahi kuchezea timu za General Tyre  na Yanga.

Makabidhiano ya vituo vya watoto yatima yamefanyika ofisini kwa Mkuu wa Mkoa ambapo Kituo cha watoto yatima kinachosimamiwa na Msikiti wa Masjid Senta kimepatiwa shilingi Milioni 5 na kituo cha watoto walemavu kilicho chini ya Kanisa Katoliki Monduli(St.John Paul Rehabilitation Center) kimepatiwa shilingi Milioni 5.

Mhe. Mkuu wa Mkoa  alifika pia nyumbani kwa mchezaji wa zamani  wa Yanga, Bw. Allan Shomari na kumkabidhi shilingi Milioni Mhe. Kimanta aliahidi  pia kutoa mchango binafsi wa shilingi laki 5 kwa Bw. Allan Shomari.

Mhe. Kimanta amesema fedha hizo alizokabidhi zimetolewa na Shirikisho la  Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kutokana na mapato yaliyopatikana kwenye mechi ya Ngao ya Hisani  kati ya timu za Simba na Namungo iliyochezwa Jijini Arusha katika  uwanja wa Sheikh Amri Abeid tarehe 30 Agosti, 2020.

 Mhe. Kimanta ameviasa vituo hivyo vya watoto kuhakikisha  fedha hizo zinatumika kwa maendeleo ya vituo vyao na si vinginevyo.

Mhe. Kimanta ameishukuru TFF kwa mchango huo wa kuwasaidia watoto wa vituo hivyo na kwa msaada walitoa kwa aliyekuwa mchezaji  wa zamani wa Timu ya Yanga, Bw. Allan Shomari.

Mhe. Kimanta ametoa  rai kwa wadau wengine kujitokeza kuvisaidia vituo vya watoto yatima na wenye ulemavu na pia kujitokeza  kumsaidia  Bw. Allan  Shomari ambaye ni mlemavu wa macho.

Akizungumza kwa niaba ya  TFF,  Mwenyekiti wa TFF Mkoa wa Arusha Bw.  Zakayo Mjema amesema  fedha hizo zimetolewa kwa vituo vya watoto yatima kama  mchango  wa TFF kwa jamii na ni imani yake kuwa vituo hivyo vinaweza kuzalisha wachezaji wazuri wa baadae kwa manufaa ya Taifa letu.

Bw. Mjema ameongeza pia kuwa michezo ina fursa mbalimbali ikiwemo ajira kwa vijana na wao kama TFF Mkoa wa Arusha wataendelea kutoa misaada kwa watoto hao ikiwemo kuwapatia mipira ya kuchezea.

Ametoa wito kwa wadau wengine kuwasaidia wachezaji wa zamani kama walichofanya kwa Bw. Allan Shomari kwa vile bado wapo wengi mitaani wanaohitaji  msaada kama huo.

Akitoa neno la shukrani, Bw. Allan Shomari  ameushukuru uongozi wa TFF  na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Kimanta kwa msaada huo waliomkabidhi ambao utamsaidia hasa kwenye matibabu yake ya Macho.


Announcements

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • View All

Latest News

  • RC MAKONDA AFUNGUA MKUTANO WA 33 WA WAKUU WA MAJESHI YA ULINZI (SADC).

    May 30, 2025
  • SAMIA MOTOCROSS CHAMPIONSHIP KUREJEA MSIMU WA PILI JULAI 12, 2025

    May 27, 2025
  • MKOA WA ARUSHA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO MKUBWA WA WAKUU WA MAJESHI WA SADC

    May 25, 2025
  • UJENZI WA UWANJA WA AFCON ARUSHA SIO MICHEZO TU, NI FURSA YA KIUCHUMI

    May 24, 2025
  • View All

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
More Videos

Quick Links

  • Guildlines Towards the use of ICT In Government
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Public Servant Portal
  • Takwimu
  • TANAPA

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

Other Contacts

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Sitemap
    • FAQ

Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.