Wafanyabiashara, Waongoza watalii na wadau mbalimbali wa Utalii Mkoani Arusha wakijumuika pamoja kuianza safari kuelekea kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa Kilimanjaro (KIA) kwaajili ya mapokezi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anayeanza ziara yake ya kikazi Mkoani Arusha leo Novemba 27, 2024.
Wadau hao wa utalii wakiongozwa na Chama cha Mawakala wa Usafirishaji Watalii Tanzania TATO wanaadhimisha miaka 40 ya kuanzishwa kwa Chama hicho wanasema wameamua kuungana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda kumlaki kwa shangwe Mhe. Rais Samia kutokana na Mchango wake mkubwa na utofauti wake katika utendaji suala lililochagiza ongezeko kubwa la watalii kwa kipindi cha miaka mitatu ya serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.