Na Elinipa Lupembe
Wafanyabiasha wadogo Jiji la Arusha, wametakiwa kukubaliana na mabadiliko ya kiuchumi yanayotokea kwa kuwa ni mabadiliko yoyote lazima yanakuja na matokeo hasi ambayo huathiri sehemu na baadhi ya watu.
Hayo yamesemwa na mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella wakati wa mkutano wa hadhara uliowakutanisha wafanyabiashara wa soko Kilombero, uliofanyika kwenye eneo la Sokoni hapo ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kukagua utekelezaji wa shughuli za maendeleo Jiji la Arusha.
Mhe. Mongela amesema hayo mara baada ya kusikiliza na kutatua kero za wafanyabiashara hao wadogo waliolalamikia ubovu wa miundombinu ya barabara za Jiji kwa baadhi ya maeneo, kuhamisishwa mara kwa mara, uchakavu wa soko hilo pamoja na mpango wa kuhamishwa stendi ya Daladala eneo la Kilombero .
Akijibu kero hizo, Mhe. Mongella ameweka wazi mpango wa serikali ya awamu ya sita ni kutekeleza awamu ya pili ya mradi mkakati wa kuboresha Miji na Majiji - TACTIC, ambao Jiji la Arusha ni miongoni mwa majiji yaliyopata neema hiyo, mradi unaotekelezwa kwa ufadhili wa Benki ya Dunia.
Ameitaja miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa kiwango cha lami barabara za kuingia na kutoka jijini, ujenzi wa soko la Kisasa stendi ya Kilombero, ujenzi wa stendi ya Daladala, ujenzi wa Standi kubwa ya mabasi yaendayo mikoni, ujenzi na soko la kisasa la Machinga eneo la stendi kubwa, miradi ambayo kimsingi yataathiri baadhi ya maeneo na baadhi ya watu.
Amewataka wafanya biashara hao kukubalina na mabadiliko yanayokuja na kuondoa hofu kwamba watakosa wateja, mabadiliko hayo yana lenga kukuza sekta ya uchumi wa mkoa wa Arusha na Tanzania kwa ujumla wake hivyo ni vema kujiandaa kuyapokea, hivyo wafanyabiasha kukubali na kujiandaa kisaikolojia kuendana na wakati.
"Hapa ilipo stendi ya Daladala linajengwa soko la kisasa la Machinga, soko ambalo nyinyi wafanya biasha ndio mtafanya biashara humo, stendi itahamia nje ya mji na Daladala zitapita katikati ya Jiji kushusha abaliria tuu, ilikupungumza msongamano wa magari, ambao ni kero kwa wananchi na unachelewesha shughuli nyingi" Ameweka wa Mhe. Mongella.
Aidha ameuagiza uongozi wa Jiji la Arusha kuweka miundombinu ya taa kwenye soko la Kilombero ili wafanyabiashara waendelee kufanya biashara mpaka usiku na kuachana na kufunga saa 12, jambo ambalo linazorotesha uchumi hoja ambayo ilitolewa na mfanyabiashara kijana Andrea Thomas
#arushafursalukuki
#KaziInaendelea
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.