Serikali inaweka mazingira wenzeshi kwa mfanyabiashara kuweza kulipa kodi kwa urahisi bila kubugudhiwa.
Yamesemwa hayo na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella alipokuwa akifungua semina ya mafunzo kwa wafanyabiashara wakubwa, Jijini Arusha.
Mpango wa Serikali si kumnyanyasa mlipa kodi au kumlazimisha alipe kodi bali ni kumfanya ailipe kwa hiara bila buguza yoyote.
Aidha, amewataka wafanyabiashara hao kuielewa mifumo yote ya ulipaji kodi ili iweze kuwarahisishia hatua zote za kupita katika kulipa kodi.
Kamishna wa walipa Kodi wakubwa kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) bwana Alfred Mregi amesema, wameboresha mifumo mbalimbali ya kulipia kodi ili kutomkandamiza mlipa kodi.
Aidha, amewataka wafanyabiashara wote wa chini, kati na juu kuendelea kulipa kodi ili kuleta maendeleo ya kweli ya Taifa.
Semina kwa wafanyabiashara wakubwa wa Mkoa wa Arusha imelenga kutengeneza ukaribu baina ya TRA na wafanyabiashara hao na kuwapa elimu ya kuielewa mifumo ya ulipaji kodi vizuri.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.