Baadhi ya wananchi wa Karatu wakiwasilisha kero zao kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Paul Christian Makonda kwenye Mkutano wa Hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Mazingira Bora Karatu mjini Mei 24, 2024
Katika mkutano huo, Mhe. Makonda amewahakikishia wananchi wa Karatu kuwa, kila mtu ambaye amepoteza Haki yake atarejeshewa na kuwasisitiza viongozi na watumishi wa Umma kuwahudumia wannachi kwa usawa bila kujali hadhi zao, tofauti zao za kiuchumi, dini wala Siasa, jambo ambalo ndilo lengo la Serikali ya awamu ya sita ya Dkt.Samia Suluhu Hassan.
"Mara nyingi nimekuwa nikimuomba Mungu anisaidie nisiungane na watu wabaya, kupokea rushwa wala kutumia nafasi yangu kunyang'anya Haki ya mtu mwingine, neno la Mungu linasema itakusaidia nini kupata umiliki wa kila duniani na kuukosa ufalme wa Mbingu?" Amebainisha Mhe. Makonda
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.