Sehemu ya vijana kutoka maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya Mkoa wa Arusha wakifanya mazoezi ya kukimbiza pikipiki kama sehemu ya kujiandaa na mashindano makubwa ya Pikipiki ya Samia Motocross Championship yanayotarajiwa kufanyika mwishoni mwa wiki hii (Julai 13-14) kwenye viwanja vya michezo vya Lakilaki Kisongo Jijini Arusha.
Mashindano haya yanasimamiwa na kuratibiwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda na mshindi wa jumla anatarajiwa kuondoka na fedha taslimu Shilingi Milioni 10, Mshindi wa pili Milioni saba na mshindi wa tatu ataondoka na Milioni tano za Kitanzania.
Mhe. Paul Christian Makonda anasema lengo la mashindano hayo ni kutekeleza kwa vitendo jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kubuni fursa nyingi zaidi za ajira kwa kutumia njia mbalimbali ikiwemo kuibua, kukuza na kustawisha vipaji na ujuzi walionao vijana wa Mkoa wa Arusha.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.