KIWANDA CHA "Kisongo Grain Market Export and Sale of Cereals and Legumes"
Kiwanda hiki kina mtambo maalumu wa kukausha mazao ya kilimo na kuyaweka mazao hayo katika ubora mzuri tayari kwa kwenda sokoni hasa masoko ya nje.
Kiwanda hiki kipya kimejikita zaidi katika Utoaji wa huduma bora ya kukausha Mazao ya Kilimo na Mifugo kabla ya kwenda katika Soko la Jumuiya ya Afrika Mashariki. Katika Ukanda ya Kaskazini, hakuna kiwanda kama hiki kitakachotoa huduma hizo. Hapo nyuma tulikuwa na kiwanda cha National Milling Corporation (NMC) ambacho kwa sasa hakipo kilichokuwa kikitoa huduma hiyo. Kwa maana hiyo, Wafanyabiashara wa Kanda ya Kaskazini hupata huduma hiyo aidha Dar-Es-Salaam au nchi jarani ya Kenya kwa gharama kubwa. Kiwanda hiki kitasaidia Mazao kabla ya kwenda katika Soko ,kupimwa na kifaa maalum ili kujua kama kuna kiwango cha ukankaji na hivyo ku0punguza sumu kavu [Afrotoxin] katika ubora wa Mazao ya Nafaka, vilevile kitasaidia kuongeza dhamani ya mnyororo kwa Wafanyabiashara na Wakulima wetu.Aidha kutusaidia katika kukausha na kuhakikisha ubora wa vyakula vya mifugo na hivyo kupunguza tatizo la sumu kavu katika mifugo.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.