Na Elinipa Lupembe
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.John V.K.Mongella amekagua mradi wa Kituo cha Afya Samunge wilaya ya Ngorongoro na kuuagiza uongozi wa wilaya na halmashauri, kufanya uchunguzi wa kina, kabla ya kutoa fedha zinazoombwa kwa ajili ya ukamilishaji wa miradi ambayo tayari serikali imetoa fedha za kuitekeleza.
Mhe. Mongella ametoa agizo hilo, mara baada ya kusomewa taarifa inayohitaji ongezeko la fedha za ukamilishaji wa baadhi ya majengo ya kituo hicho cha afya, huku tayari Serikali Kuu, ilishatoa fedha za ujenzi, zikiwa na maelekezo ya kukamilisha ujenzi wa majengo.
"Wakuu wa wilaya na wakurugenzi msikubali kuongeza fedha zinazoombwa na wasimamizi wa miradi, kabla ya kuzito, fanyeni uchunguzi wa kina ili kujiridhisha endapo kiasi cha fedha kinachoombwa ni sahihi ama la, pamoja na kufahamu sababu za kutokukamilisha mradi wakati tayari serikali ilikwisha kutoa fedha zikiwa na maelekezo ya kukamilisha mrafi" Amesema Mhe. Mongella.
Aidha ameendelea kukemea tabia ya baadhi ya halmashauri kushindwa kukamilisha miradi kwa fehda zilizoletwa na Serikali Kuu, na kuongeza fedha kupitia mapato ya ndani na kuwataka wakuruge zi kuacha mara moja tabia hiyo kwa kusisitiza kuwa kila fedha inakuja na maelekezo ya kukamilisha mradi kwa halmashauriz ote nchini huku akihoji kwanini wengene wakamilishe kwa kiasi hicho cha fedha na wengine wasikamilishe,
Awali serikali ilitoa fedha kiasi cha shilingi milioni 400 kwa ajili ya kupanua zahanati hiyo ya Sambunge na kuwa kituo cha afya na tayari kimeanza kutoa huduma za kulaza kwa wanawake wajawazitona kuongeza kiasi cha shilingi milioni 100 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba.
#tutakufikiapopoteulipoArusha
#KaziInaendelea
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.