Na Elinipa Lupembe
Wakuu wa Idara za Utawala na Rasilimaliwatu wametakiwa kusimamia majukumu yao kwa mujibu wa sheria kwa kuzingatia viapo vya Utumishi wa Umma walivyoapa kusimamia na kuwahudumia watumishi wa Umma kwa kuzingatia Kanuni sheria na taratibu za utumishi.
Rai hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene, wakati akifungua mkutano wa mwaka wa viongozi hao uliofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Arusha (AICC) mkoani Arusha.
Mhe. Simbachawene ameweka wazi kuwa kutokana na utafiti uliofanywa na Wizara yake mwaka 2022, umebaini kuna maeneo Maafisa Raslimaliwatu hawatekelezi majukumu yao kulingana na viapo vyao ambavyo vinawawezesha kuwa na Utumishi uliotukuka ili kufikia malengo ya taasisi zao na serikali kwa ujumla.
Amesisitiza kufanyia kazi matokeo ya tafiti hiyo kwa maafisa hao kufanya kazi kwa weledi kwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo, chukueni hatua katika kuboresha utawala na usimamizi wa rasilimali watu katika maeneo yenu.
Hata hivyo amekemea tabia ya baadhi ya Maafisa Tawala matumizi mabaya ya madaraka ikiwemo upendeleo, matumizi binafsi Katika Utumishi jambi ambalo limedidimiza na kukwamisha taasisi kufikia malengo na kuwataka maafisa hao kujitathimini na kiwacha tabia hizo.
"Kuna maeneo ya ambayo Maafisa Rasilimaliwatu wanalegalega katika kusimamia Sera,kanuni, sheria, maadili na miongozo,huo sio utendaji unaoridhisha kwa kuwa kuna watumishi wengi hawawajibiki ipasavyo na kutahadharisha kwamba eneo litakalobainika lina mapungufu, Serikali haitasitaa kuwachukulia hatua hivyo kabla hawakachukukuwa hatua wakatekeleze majukumu yao ipasavyo.
Ameongeza kuwa ofisi yake imekuwa ikipokea malalamiko ya watumishi Wastaafu hivyo akawataka maafisarasilimali watu wawe wanakaa na watumishi wanaokaribia kustaafu Ili kuwapatia elimu wawaandae vizuri,wawasilishe michango yao mapema Ili wanapostaafu wasisumbike ,wasiteseke na hatimae kufariki mapema wakihangaika mafao yao.
Naye Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Xavier Daudi, amebainisha kwa, lengo la kikao kazi hicho kukumbushana utekelezaji wa majukumu yao, kujadili changamoto zinazokwamisha utekelezaji na namna ya kuzitatua, kupeana maelekezo pamoja na kubadilishana uzoefu katika utekelezaji wa majukumu ya kazi kwa kuzingatia shabaha na vipaumbele vya kiataifa.
Aidha amewapongeza watendaji hao kwa kazi kubwa wanayoifanya watalamu hao, kwa utekelezaji wa majukumu yenu ya siku hasi siku, ninawapongeza watendaji wa ofisi yangu, ndio yenye dhamana Rasilimali kiongozi katika raismali nyingi nchini ni fusa sahihi ya kupeana maelekezipo na kujadiliana juu ya ustawi wa sekata hii muhimu ya maendeleo ya nchi yetu, uongozi wa mkoa wa Arusha kwa mapokezi.
Hata hivyo mkuu wa mkoa Arusha Mhe. John Mongela licha ya kuwakaribisha kwenye mkoa wa Arusha,
Maafisa Tawala kufurahia mandhari na hali ya hewa nzuri ambayo watu kutoka mataifa mbalimbali hufika mkoani Arusha na kufurahia.
Aidha amewahimiza watalamu hao, kuhakikisha wanapata wasaa wa kufanya utalii wa ndani kwa kutembelea vivutio vya Utalii ndani ya mkoa wa Arusha ili kumuunga mkono Rais Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassani kwa kampeni yanu ya kimataifa ya Royal Tour.
Kikao kazi hicho cha Wakuu wa Idara za Utawala na rasilimali watu Katika Utumishi wa umma kimeandaliwa na ofisi ya Rais,manegmenti ya Utumishi wa umma na utawala bora kauli mbiu yake inasema Usimamizi wa raslimali watu unaozingatia maadili,Sheria na uwajibikaji na matumizi ya tehama ni msingi wa huduma bora Katika Utumishi wa umma.
#arushafursalukuki
#kaziinaendelea
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.