Mkuu wa Wilaya ya Karatu Mhe. Dadi Kolimba amesema Wilaya yake imefanya vizuri katika kutekeleza miradi ya wananchi kupitia mfuko wa kunusuru kaya maskini (TASAF) imetokana na ushirikiano uliopo baina ya viongozi, wataalamu na wananchi.
Ameyasema hayo alipokuwa akikagua miradi ya wananchi iliyotekelezwa na TASAF awamu ya nne katika ziara maalumu ya kujengeana uelewa wa pamoja kwa viongozi wa Wilaya, Halmashauri na waratibu wa TASAF ngazi za Halmshauri.
"Kufanya kazi kwa ushirikiano ndio kumepelekea miradi hii kukamilika kwa kiwango kikubwa na kwa ubora".
Aidha, Mhe. Kolimba amesema miradi mingi imeibuliwa na wananchi wenyewe kwenye maeneo yao kutokana na changamoto wanazokuwa wanakutana nazo.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Mhe. Raymond Mangwala amesema amefurahishwa na miradi ya TASAF Wilayani Karatu imefanikiwa kwa kiwango kikubwa.
Wamejifunza kushirikiana kwa ukaribu zaidi kati ya Serikali na wananchi ili kutambua na kukamilisha miradi kwa wakati.
Aidha, Mhe. Mangwala amewashauri wataalamu kutoka TASAF Makao Makuu kuangalia zile Halmashauri zinazofanya kazi vizuri kuziongezea fedha za miradi mingi zaidi ili iwe kama motisha kwa wengine kufanya vizuri zaidi.
Amewahasa waendelee kutunza miradi hiyo ili ilete manufaa zaidi kwa wananchi.
Ziara ya kukagua miradi ya TASAF kwa Mkoa wa Arusha imefanywa kwa lengo la kujengeana uelewa wa pamoja kuhusu utekelezaji wa miradi hiyo kwa ngazi ya Mkoa na Halmashauri.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.