Na Elinipa Lupembe
Wanafunzi wametakiwa kutumia muda wao vizuri kwa kusoma kwa bidii ili kupata ujuzi na maarifa kwa kuwa serikali imewekeza fedha nyingi kwenye miundombinu ya sekta ya elimu ili kuwa na mazingira bora ya kujifunzia na kufundishia kwa wanafunzi na walimu.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. John V.K. Mongella wakati alipotembelea shule ya wasichana Arusha na kupata fursa ya kuwafundisha wanafunzi wa kidato cha sita somo la Uchumi.
Mhe. Mongella amesema kuwa licha ya serikali kutoa elimu bila malipo imeenda mbali zaidi kwa kuwekeza na kufanya maboresho makubwa kwenye miundombinu ya elimu, lengo likiwa ni kuzalisha watalamu wa fani mbalimbali ambao watakuja kulitumikia Taifa la Tanzania.
"Serikali ya awamu ya sita imetoa fursa kwa kila mtoto wa kitanzania kusoma, imetekeleza miradi mingi ya elimu, imeajiri walimu sasa kazi kubwa iliyobaki ni ninyi wanafunzi kutumia fursa hii kusoma kwa bidii na kupata ujuzi na maarifa sambamba na kufikia ndoto za kuwa watalamu wabobezi wa nchi yetu" Amesema Mkuuu huyo wa mkoa.
Aidha amewasihi wanafunzi hao kuwa na uelewa wa masomo wanayosoma kwa kuyahusianisha na maisha yao ya kila siku jambo ambalo litawafanya kuweza kutumia taaluma zao katika kulitumikia Taifa.
Hata hivyo Mhe. Mongela aliwauliza wanafunzi hao wanawezaje kuhusianisha somo la Uchumi na maisha ya kawaida sambamba na miundombinu ya madarasa na mabweni inayojengwa na serikali shuleni hapo.
Marry Joseph Kuandika amesema kuwa, uwekezaji wa miundombinu katika shule ya wasichana Arusha, umelenga kuwainua wasichana kielimu ili kujenga usawa kati ya wasichana na wavulana kutokana na 'gape' lililokuwepo hapo awali ambapo wavulana peke yao ndio walipata fursa ya kusoma kuliko wasichana.
Ameongeza kuwa msichana ni mama, ambaye kiasili ndiye mlezi wa familia na Taifa pia, hivyo ukimuelimisha mwananmke umeielimisha jamii, serikali inawaanda wasichana ambao watakuwa walezi wa jamii iliyokombolewa kifkra kupitia elimu waliyoipata.
"Tunamshukuru Rais wetu mama Samia Suluhu Hassan kwa kutujali wasichana wa Tanzania, tunaamini analiongoza taifa letu kwa upendo kama mama anayetamani kila mtoto wake afanikiwe kila kitu" Amesema Marry Joseph
Awali kuelekea miaka mitatu ua awamu ya sita, mkoa wa Arusha unatekeleza miradi ya elimu kupitia Miradi ya UVIKO 19, Kapu la mama, SEQUIP, BOOST na EP4R miradi ambayo imeboresha miundombinu ya shule, nyu,ba za walimu pamoja na uendeshaji wa shule unaochangia kupanda kwa kiwango cha taaluma.
#ArushaFursaLukuki
#KaziInaendelea
PICHA
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.