Na Elinipa Lupembe
Wanafunzi mkoani Arusha wametakiwa kujenga tabia ya kushiriki michezo mbalimbali wawapo shuleni, kwa kuwa michezo huchangamsha mwili na akili ya binadamu na kumuongezea uwezo wa kufikiriki na kuchagiza hali ya mwanafunzi kujifunza.
Rai hiyo, imetolewa na Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. John V.K Mongella, wakati akikabidhi mipira 1000 ya mchezo wa soka kwenye shule za msingi na sekondari za mkoa huo, iliyotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani - FIFA, kupitia Chama cha Mpira wa Miguu Tanzania - TFF, kwa lengo la kuendeleza michezo shuleni pamoja na kuibua na kukuza vipaji vya wanafunzi.
Mhe. Mongella, amewasisitiza wanafunzi kushiriki michezo wawapo shuleni, kwa kuwa upo uhusiano mkubwa kati ya michezo na akili ya mwanafunzi katika uwezo wa kufikiri na kumuwezesha kufanya vizuri kwenye masomo licha ya kuwa michezo hujenga afya.
"Tunapaswa kutambua michezo ni afya, kila mmoja wetu ajenge tabia ya kushiriki michezo kwa kuwa huufanya mwili kuchangamka na kuondoa ugoigoi zaidi michezo huamsha akili na kuongeza uwezo wa kufikiri hivyo kwa wanafunzi michezo huongeza na kuamsha uwezo wa kufujifunza, upo uhusiano chanya kati ya michezo na masomo" Amesisitiza Mkuu huyo wa Mkoa
Aidha, amewasisitiza Maofisa Elimu wa ngazi zote kwa kushirikiana na walimu kuwasimamia kutumia mipira hiyo kwa malengo yaliyokusudiwa ya kuendeleza soka shuleni pamoja na kuhakukisha wanafunzi wanashiriki michezo na kupata timu za kushiriki mashindano ya ngazi zote mpata Taifa na Kimataifa
Hata hivyo, amemeishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya Jemadari Dkt. Samia kwa kundeleza michezo shuleni, licha ya kuwekeza fedha nyingi kwenye kuboresha miundombinu ya shule, ameenda mbali zaidi kwa kutoa mipira kwa wananfunzi ili kuendeleza michezo shuleni.
Serikali ya awamu ya sita imewe historia kwenye sekta ya michezo, Mhe. Rais ametoa hamasa kwenye soka, tumeshuhudia Timu ya Taifa ikisonga mbele, huku vilabu vikubwa nchini vya Simba na Yanga, vikiingia robo fainali kwenye mashindano ya kimataifa, historia ambayo haijawahi kutokea.
Katika program ya FIFA ya kuendeleza michezo shuleni kupitia TFF, Mkoa wa Arusha umepokea mipira 1000 kwa ajili ya shule 100 za Msingi na Sekondari katika Halmashauri zozotsaba za Mkoa wa Arusha, ambapo kila shule iliyoainishwa imepata mipira 10.
#ArushaFursaLukuki
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.