Jumla ya wanafunzi 42 kati ya wanafunzi 87 walipoangiwa kujiunga na kidato cha kwanza shule ya sekondari Meserani wilaya ya Monduli, mkoa wa Arusha, wameripoti na kuanza masomo tarehe 08 Januari, 2024.
Wanafunzi hao, wamekiri kufurahia kuchaguliwa na Serikali kujiunga na kidato cha kwanza shule ya sekondari Meresrani, shule ambayo wamekiri ina miundombinu bora inayowafanya kujisikia fahari kubwa.
"Tunafurahia kusoma kwenye shule nzuri, madarasa ni mazuri kama shule za 'private', tunamshukuru Mama Samia na tunaahidi kusoma kwa bidii na kufika ndoto zetu pamoja na kutimiza malengo ya Serikali"
#arushafursalukuki
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.