Wanafunzi wa shule ya Msingi Emairete, wakiwa na miti ambayo wamekabidhiwa na Mkuu wa Wilaya ua Monduli Mhe. Festo Shemu Kiswaga kwa ajili ya kuipanda na kuitunza wakati wate wawapo shuleni.
Wanafunzi hao, wamekabidhiwa miti hiyo, wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Upandaji Miti Mkoa wa Arusha, yaliyofanyika kwenye shule ya Msingi Emairete, kijiji cha Emairete kata ya Monduli Juu, wilaya ya Monduli leo Aprili 03, 2024.
Hata, Mkuu huyo wa wilaya amewataka wanafunzi hao kujifunza kupanda miti na kuitunza ikiwa ni jukumu lao la kutunza mazingira yanayowazunguka, na kusisitiza kuwa jukumu la kupanda na kutunz amazingira ni la kila mwananchi kuanzia ngazi ya familia ambapo inahusisha malezi na makuzi ya watoto wanajali mazingira yao.
Awali, wakiimba shairi, wanafunzi hao, wamemuahisi Mkuu huyo wa wilaya kuitunza miti hiyo kwa kuwa wao ni mabalozi wa mazingira na tayari wanao uelewa mkubwa juu ya uhusiano wa miti na mazingira na maisha ya binadamu na viumbe viishivyo duniani.
Kauli Mbiu ya mwaka 2024: "Misitu ni Ubunifu"
#ArushaFursaLukuki
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.