• Complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Arusha Regional

The United Republic of Tanzania President Office Regional Administration and Local Government Arusha Regional

  • Home
  • About Us
    • History
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa mikoa waliopita-Arusha
    • Dira na dhima
    • The basics
    • Strategies
  • Administration
    • Structure
    • Departments
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Units
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • District
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Councils
    • Arusha CC
    • Arusha DC
    • Meru DC
    • Monduli DC
    • Karatu DC
    • Longido DC
    • Ngorongoro DC
  • Investment Opportunities
    • Tourism
    • Livestock
    • Agricultre
    • Industrial
  • Our Service
    • Health
    • Education
    • Water
    • Land
    • Tourism
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events

WANANCHI 367 WAHAMA HIFADHI YA NGORONGORO.

Posted on: August 22nd, 2024

Na Mwandishi wetu, Ngorongoro 


Muitikio wa wananchi wanaoishi katika eneo la hifadhi ya Ngorongoro kuendelea kuhama kwa hiari umepamba moto ambapo leo tarehe 22 Agosti, 2024 jumla ya kaya 79 zenye watu 367 na mifugo 995 zimehama kutoka hifadhi ya Ngorongoro kwenda Kijiji cha Msomera Handeni na maeneo mengine waliyochagua wenyewe.


Akiwaaga wananchi hao Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya Maliasili na Utalii (anayesimamia maliasili) CP Benedict Wakulyamba amesema kuwa kuondoka kwa kundi hilo leo ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wa kulinusuru eneo la hifadhi ya Ngorongoro ambapo wananchi wameendelea kuelimishwa na kuhama kwa hiari kwa ajili ya kuboresha maisha yao na kunufaika na fursa za kiuchumi zilizoko nje ya hifadhi.


Ametoa tahadhari kuwa wapo baadhi ya wananchi ambao wamekuwa wakihamia Msomera kinyemela bila kufuata utaratibu uliowekwa na kuleta changamoto kwa ndugu zao wanaowakuta huko na kuwasihi kuwa kufuata utaratibu na miongozo iliyowekwa ili wawe wakazi halali wa maeneo wanayopenda kuhamia.


Akitoa taarifa ya utekelezaji wa mpango wa kuhamisha wananchi wa Ngorongoro kwa hiari, Afisa Uhifadhi mkuu na Meneja mradi wa kuhamisha wananchi kwa hiari PCO Flora Assey amebainisha kuwa tangu zoezi hilo lilipoanza mwezi Juni, 2022 hadi kufikia mwezi Agosti, 2024 takriban kaya 1,598 zenye watu 9,618 na mifugo 39,779  imeshahama ndani ya hifadhi kwenda Kijiji cha Msomera na maeneo mengine.


Akiongea kwa niaba ya Kamishna wa Uhifadhi, Kamishna msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi Mhandisi Daniel Chegere ameeleza kuwa NCAA inaendelea na zoezi la kuwaelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa kuhama kwa hiari katika eneo la hifadhi na kwenda maeneo yaliyotengwa na Serikali kwa kujengewa miundombinu ya kisasa yenye huduma zote muhimu za kijamii ambazo ni salama zaidi tofauti na ilivyo ndani ya ya hifadhi. 


Mhandisi Chegere ameongeza kuwa hali ya usalama katika hifadhi hiyo inaendelea vizuri, ambapo ulinzi umeimarishwa na wageni mbalimbali wanaotembelea hifadhi hiyo wanaendelea na shughuli za utalii bila changamoto.


Announcements

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • View All

Latest News

  • RC MAKONDA AFUNGUA MKUTANO WA 33 WA WAKUU WA MAJESHI YA ULINZI (SADC).

    May 30, 2025
  • SAMIA MOTOCROSS CHAMPIONSHIP KUREJEA MSIMU WA PILI JULAI 12, 2025

    May 27, 2025
  • MKOA WA ARUSHA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO MKUBWA WA WAKUU WA MAJESHI WA SADC

    May 25, 2025
  • UJENZI WA UWANJA WA AFCON ARUSHA SIO MICHEZO TU, NI FURSA YA KIUCHUMI

    May 24, 2025
  • View All

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
More Videos

Quick Links

  • Guildlines Towards the use of ICT In Government
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Public Servant Portal
  • Takwimu
  • TANAPA

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

Other Contacts

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Sitemap
    • FAQ

Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.