Na Daniel Gitaro
Ikiwa ni kilele cha maadhimisho ya wiki ya huduma za kifedha, Wananchi wa Mkoa wa Arusha, wamejitokeza kwa wingi kutembelea na kupata elimu ya huduma za kifedha kwenye mabanda mbalimbali ya watoa huduma hizo na kuvuka lengo lililokuwa limewekwa la kufikia wananchi elfu nane.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Felician Mtahengerwa alipokuwa akihitimisha maonyesho hayo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John V.K. Mongella, ambapo wananchi zaidi ya elfu kumi walijitokeza kushiriki maonyesho hayo na kupata elimu ya huduma za kifedha.
Aidha, amesema kuwa, utoaji wa elimu hiyo utasaidia wananchi kupata uelewa juu ya elimu ya fedha na kufikia lengo lililowekwa la kufikia asilimia 80 ya wananchi kufikiwa na huduma hiyo ifikapo mwaka 2025.
“Ni matumaini yangu kuwa elimu iliyotolewa kupitia maadhimisho haya itawawezesha wananchi walio wengi kutumia huduma za kifedha zilizo rasmi na kwa ufanisi ili kuboresha maisha yenu kupitia shughuli mbalimbali za kiuchumi”. Amesema.
Kwa upande wake Kamishina wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha Dkt. Charles Mwamwaja amesema kuwa lengo kuu ya maadhimisho hayo ni kutoa elimu kwa wananchi kuhusu utumiaji wa huduma za kifedha, jambo ambalo limefanyika wakati wa maadhimisho hayo.
Ameongeza kuwa, Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na wadau mbalimbali na watoa huduma za kifedha, wataendelea kutoa programu hizo za mafunzo ka kutumia njia na mbinu mbalimbali na hatimaye kuwafikia wananchi wengi Zaidi.
“Tunaamini elimu hii imewafikia watanzania wengi, lakini elimu inakuwa ina maana sana kama itakusaidia kubadilisha maisha yako na kubadilisha namna ambayo ulikuwa ukiishi hapo awali kabla ya kupata elimu, hivyo ni vyema wananchi mkazingitie yale mliyoyapata hapa kwa manufaa ya shughuli zenu za kimaendeleo”.
Hata hivyo, baadhi ya watoa huduma za kifedha walioshiriki kwenye maonyesho hayo wamethibitisha uwepo wa uhaba wa elimu ya masuala ya kifedha kwa wananchi walio wengi hali inayosababisha kujiingiza kwenye mikopo inayowaumiza.
Nao baadhi ya wananchi waliohudhuria wakati wa kilele cha maadhimisho hayo wamesema wamefurahishwa sana huduma hiyo kwani wamepata elimu ya msingi sana itakayowasaidia kuweka akiba na kutengeneza faida kutokana na shughuli zao za maendeleo.
“Maonyesho haya yamekuwa na manufaa makubwa sana kwetu hasa wakazi wa Arusha kwasababu tumepata elimu mbalimbali kuhusu masuala ya kifedha, kukopa na kuweka akiba, namna ya kukua kiuchumi kupitia vikundi vidogo vidogo pamoja na Sheria za kifedha”. Amesema Lazaros Laizer.
Awali, maonyesho ni ya tatu kufanyika kitaifa, na kuleta mafanikio makubwa Zaidi ya maonyesho yliyofanyika hapo awali Jijini Dar-es-salaam na jijini
#arushafursalukuki
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.